Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Juni 2027 › 11 Juni

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 11 Juni 2027

Ijumaa · Juma la 10 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Ijumaa ya Juma la 10 la Mwaka

Kumbukumbu · Rangi ya liturujia: nyekundu

Mt. Barnaba, mtume · Kumbukumbu

Kufunga na toba

Siku ya toba

Kila Ijumaa ni siku ya toba; kila baraza la maaskofu huamua jinsi inavyoadhimishwa: kujinyima nyama au tendo lingine la toba. Kufunga kunawahusu wenye miaka 18 hadi 59, kujinyima nyama kuanzia miaka 14.

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Mdo 11:21–26; 13:1–3

21Na mkono wa Bwana ulikuwa pamoja nao, na watu wengi waliamini na kumgeukia Bwana. 22Habari zao zikafikia masikioni mwa kanisa la Yerusalem: na wakamtuma Barnaba aende mpaka Antiokia. 23Alipokuja na kuona karama ya Mungu alifurahi; na aliwatia moyo wote kubaki na Bwana katika mioyo yao. 24Kwa sababu alikuwa mtu mwema na amejazwa na Roho Mtakatifu na imani na watu wengi wakaongezeka katika Bwana. 25Baadaye Barnaba alienda Tarso kumwona Sauli. 26Alipompata, akamleta Antiokia. Ikawa kwa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi wakaitwa wakristo kwa mara ya kwanza huko Antiokia. 13:1Sasa katika kanisa la Antiokia, palikuwa na baadhi ya manabii na walimu. Walikua Barnaba, Simeoni (aliyeitwa Nigeri). Lukio wa Kirene, Manaeni(ndugu asiye wa damu wa Herode kiongozi wa mkoa), na Sauli. 2Walipokuwa wakimwabudu Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu alisema, “Niteengeeni pembeni Barnaba na Sauli, waifanye kazi niliyo waitia.” 3Baada ya Kanisa kufunga, kuomba, na kuweka mikono yao juu ya watu hawa, wakawaacha waende.

Wimbo wa katikati

Zab 116:10–11, 15–18

10Nilimwamini yeye, hata niliposema, “nimeteswa sana.” 11Kwa haraka nilisema, “Watu wote ni waongo.” 15Mauti ya wacha Mungu ina thamani machoni pa Mungu. 16Ee Yahwe, hakika, mimi ni mtumishi wako; mimi ni mtumishi wako, mwana wa mjakazi wako; umefungua vifungo vyangu. 17Nitakutolea dhabihu ya shukrani na nitaliitia jina la Yahwe. 18Nitatimiza viapo vyangu kwa Yahwe katika uwepo wa watu wake wote,

Injili

Mt 5:27–32

27Mmesikia imenenwa kuwa, 'Usizini.' 28Lakini nawaambieni yeyote amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naye moyoni mwake. 29Na kama jicho lako la kulia linakusababisha kujikwaa, ling'oe na ulitupe mbali nawe. Kwa kuwa ni afadhali kiungo kimoja katika mwili wako kiharibike kuliko mwili mzima kutupwa jehanamu. 30Na kama mkono wako wa kuume unakusababisha kujikwaa, ukate kisha uutupilie mbali nawe. Maana ni afadhali kiungo kimoja katika mwili wako kiharibike kuliko mwili mzima kutupwa jehanamu. 31Imenenwa pia, yeyote amfukuzaye mkewe, na ampe hati ya talaka.' 32Lakini mimi nawaambia, yeyote anaye mwacha mke wake, isipokuwa kwa kwa sababu ya zinaa, amfanya kuwa mzinzi. Na yeyote amuoaye baada ya kupewa talaka afanya uzinzi.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 11 Juni

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki