Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Mei 2027 › 28 Mei
Kalenda ya Kiorthodoksi · 15 Mei (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 28 Mei 2027
Ijumaa · Wiki ya 4 ya Pasaka · Sauti ya 3
Sikukuu na watakatifu
Mtakatifu Mtawa Pakomio Mkuu (karibu 348)
Siku ya mfungo
Samaki wanaruhusiwa
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
44Wakati Petro akiendelea kusema haya, Roho Mtakatifu akawajaza wote waliokuwa wakisikiliza ujumbe wake. 45Watu wale wanaohusika na kikundi cha waamini waliotahiriwa- wale wote waliokuja na Petro- walishangazwa, kwa sababu ya karama ya Roho Mtakatifu aliyemwagwa pia kwa wamataifa. 46Kwa kuwa walisikia hawa wamataifa wanaongea kwa lugha zingine na kumwabudu Mungu. Petro akajibu, 47“Kuna mtu yeyote anaweza kuzuia maji ili watu wasibatizwe, Watu hawa wamempokea Roho Mtakatifu kama sisi?” 48Ndipo akawaamuru wabatizwe kwa jina la Yesu Kristo. Baadaye wakamwomba akae nao kwa siku kadhaa. 11:1Mitume na ndugu wale waliokuwa huko Yudea walisikia kuwa wamataifa wamelipokea neno la Mungu. 2Petro alipokuja huko Yerusalemu, lile kundi la watu waliotahiriwa wakaanza kumkosoa, Wakisema, 3“Umeshikamana na watu wasiotahiriwa na kula nao!” 4Lakini Petro alianza kueleza tukio kwa kina; akisema, 5“Nilikuwa naomba katika mji wa Yafa, na nikaona maono ya chombo kikishuka chini kama nguo kubwa ikishuka kutoka mbinguni katika pembe zake zote nne. Kikashuka kwangu. 6Nilikitazama na kufikiri juu yake. Nikaona wanyama wenye miguu minne waishio katika nchi, na wanyama wa polini na wanyama watambaao na ndege wa angani. 7Kisha nikasikia sauti ikisema nami, “Amka, Petro, chinja naj ule!” 8Nikasema, “Siyo hivyo, Bwana, mdomoni mwangu hakujawahi kuingia kitu chochote kisicho kitakatifu au kichafu” 9Lakini sauti ikajibu tena kutoka Mbinguni, kile Mungu alichokitangaza kuwa ni safi, usikiite najisi, 10Hii ilitokea mara tatu, na kila kitu kikachukuliwa mbinguni tena.
Injili
21Basi akawaambia tena, “Ninaenda zangu; mtanitafuta na mtakufa katika dhambi zenu. Kule niendako, hamuwezi kuja.” 22Wayahudi wakasema, “Atajiua mwenyewe, yeye ambaye alisema, 'kule niendako hamuwezi kuja'?” 23Yesu akawaambia, “Mnatoka chini; mimi natoka juu. Ninyi ni wa Ulimwengu huu; mimi si wa ulimwengu huu. 24Kwa hiyo, naliwaambieni kuwa mtakufa katika dhambi zenu. Vinginevyo muamini kuwa MIMI NDIYE, mtakufa katika dhambi zenu”. 25Kwa hiyo wakamwambia, “Wewe ni nani?” Yesu akawaambia, Yale niliyowaambia tangu mwanzo. 26Ninayo mambo mengi ya kuzungumza na kuhukumu juu yenu. Hata hivyo, yeye aliyenituma ni wa kweli; na mambo niliyoyasikia kutoka kwake, mambo haya nayasema kwa Ulimwengu.” 27Hawakumuelewa kwamba alikuwa akiongea nao kuhusu Baba. 28Yesu akasema, “Mtakapomwinua juu Mwana wa Mtu, ndipo mtakapojua kuwa MIMI NDIYE, na kwamba sifanyi lolote kwa nafsi yangu. Kama Baba alivyonifundisha, ninazungumza mambo haya. 29Yeye aliyenituma yuko pamoja nami, na yeye hajaniacha peke yangu, kwani kila mara nafanya yale yanayompendeza.” 30Wakati Yesu akisema mambo haya, wengi walimwamini.
Watakatifu wa siku
- Askofu Mtakatifu Isaya, Askofu wa Rostov, mtenda miujiza (1090)
- Mwana wa Mfalme Mwaminifu Demetrio, mrithi wa kiti cha ufalme, wa Uglich na wa Moscow (1591)
- Mtakatifu Mtawa Isaya wa Mapango ya Kyiv (1115)
- Mtakatifu Mtawa Pakomio wa Nerekhta (1384)
- Watakatifu Watawa Eufrosino na mwanafunzi wake Serapioni, wa Pskov (1481)
- Mtakatifu Mtawa Akilio, Askofu wa Larisa (karibu 330)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 15 Mei katika kalenda ya kanisa ni 28 Mei katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki