Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Mei 2027 › 28 Mei

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 28 Mei 2027

Ijumaa · Juma la 8 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Ijumaa ya Juma la 8 la Mwaka

Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: kijani

Kufunga na toba

Siku ya toba

Kila Ijumaa ni siku ya toba; kila baraza la maaskofu huamua jinsi inavyoadhimishwa: kujinyima nyama au tendo lingine la toba. Kufunga kunawahusu wenye miaka 18 hadi 59, kujinyima nyama kuanzia miaka 14.

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Haimo katika tafsiri hii

Wimbo wa katikati

Zab 149:1–6, 9

1Msifuni Yahwe. Mwimbieni Yahwe wimbo mpya; imbeni sifa zake katika kusanyiko la waaminifu. 2Israeli ishangilie katika yeye aliye iumba; watu wa Sayuni na washangilie katika mfalme wao. 3Nao walisifu jina lake kwa kucheza; na wamuimbie sifa yeye kwa ngoma na kinubi. 4Kwa kuwa Yahwe hupata furaha katika watu wake; huwapa utukufu wanyeyekevu kwa wokovu. 5Wacha Mungu wauchangilie ushindi; nao waimbe kwa furaha vitandani mwao. 6Sifa za Mungu na ziwe vinywani mwao na panga mbili zenye makali mkononi mwao 9Hii itakuwa ni heshima kwa ajili ya watakatifu wake wote. Msifuni Yahwe.

Injili

Mk 11:11–26

11Ndipo Yesu aliingia Yerusalemu na alikwenda hekaluni na alitazama kila kitu. Sasa, wakati ulikuwa umeenda, alikwenda Bethania pamoja nao kumi na wawili. 12Siku iliyofuata, wakati walipokuwa wakirudi kutoka Bethania, alikuwa na njaa. 13Na akaona mti wa mtini uliokuwa na majani kwa mbali, alikwenda kutazama kama angeweza kupata chochote juu yake. Na wakati alipokwenda kwa huo, hakupata chochote isipokuwa majani, kwa kuwa haikuwa majira ya mtini. 14Aliuambia, “Hakuna yeyote atakayekula tunda kutoka kwako tena”. Na wanafunzi wake wakasikia. 15Walikuja Yerusalemu, naye aliingia hekaluni na kuanza kuwatoa nje wauzaji na wanunuzi ndani ya hekalu. Alizipindua meza za wabadilishaji wa fedha na viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa. 16Hakumruhusu yeyote kubeba chochote hekaluni kilichoweza kuuzwa. 17Aliwafundisha na akasema, “Je haikuandikwa, 'nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote'? Lakini mmeifanya pango la wanyang'anyi”. 18Makuhani wakuu na waandishi walisikia alivyokuwa amesema, nao walitafuta njia ya kumwua. Hata hivyo walimwogopa kwa sababu umati ulishangazwa na mafundisho yake. 19Na kila wakati jioni ilipofika, waliondoka mjini. 20Walipokuwa wakitembea asubuhi, waliuona mti wa mtini umekauka mpaka kwenye mizizi yake. 21Petro alikumbuka na kusema, “Rabi! Tazama, mti wa mtini ulioulaani umekauka”. 22Yesu aliwajibu, “Muwe na imani katika Mungu. 23Amini nawaambia kwamba kila auambiaye mlima huu, 'Ondoka, na ukajitupe mwenyewe baharini, 'na kama hana mashaka moyoni mwake lakini anaamini kwamba alichokisema kitatokea, hivyo ndivyo Mungu atakavyofanya. 24Kwa hiyo ninawaambia: kila kitu muombacho na kuuliza kwa ajili yake, aminini kwamba mmepokea, navyo vitakuwa vyenu. 25Wakati mnaposimama na kuomba, mnapaswa kusamehe chochote mlichonacho dhidi ya yeyote, ili kwamba Baba yenu aliye mbinguni awasamehe pia ninyi makosa yenu.

Watakatifu wa 28 Mei

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki