Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Mei 2027 › 15 Mei
Kalenda ya Kiorthodoksi · 2 Mei (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 15 Mei 2027
Jumamosi · Wiki ya 2 ya Pasaka · Sauti ya 1
Sikukuu na watakatifu
Askofu Mtakatifu Athanasio Mkuu, Askofu Mkuu wa Aleksandria († 373)
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
21Waliposikia hili, waliingia hekaluni wakati wa kupambazuka na kufundisha. Lakini, kuhani mkuu alikuja na wote waliokuwa naye, na kuitisha baraza lote kwa pamoja, na wazee wote wa watu wa Israeli, na kuwatuma gerezani ili kuwaleta mitume. 22Lakini watumishi waliokwenda, hawakuwakuta gerezani, walirudi na kutoa taarifa, 23“Tumekuta gereza limefungwa vizuri salama, na walinzi wamesimama langoni, lakini tulipokuwa tukifungua, hatukuona mtu ndani.” 24Sasa wakati jemedari wa hekalu na makuhani wakuu waliposikia maneno haya, waliingiwa na shaka kubwa kwa ajili yao wakiwaza litakuwaje jambo hili. 25Kisha mmoja akaja na kuwaambia, “Watu mliowaweka gerezani wamesimama hekaluni na wanafundisha watu.” 26Hivyo jemedari alienda pamoja na watumishi, na wakawaleta, lakini bila ya kufanya vurugu, kwa sababu waliwaogopa watu wangeweza kuwapiga kwa mawe. 27Walipokwisha kuwaleta, waliwaweka mbele ya baraza. Kuhani mkuu aliwahoji 28akisema, “Tuliwaamuru msifundishe kwa jina hili, na bado mmeijaza Yerusalemu kwa fundisho lenu, na kutamani kuleta damu ya mtu huyu juu yetu.” 29Lakini Petro na mitume wakajibu, “Lazima tumtii Mungu kuliko watu. 30Mungu wa baba zetu alimfufua Yesu, mliyemuua, kwa kumtundika juu ya mti. 31Mungu alimtukuza katika mkono wake wa kuume, na kumfanya kuwa Mkuu na mwokozi, kutoa toba kwa Israeli, na msamaha wa dhambi. 32Sisi ni mashahidi wa mambo haya, na Roho Mtakatifu, ambaye Mungu amemtoa kwa wale wanaomtii.” 33Wajumbe wa baraza waliposikia hivi, walishikwa na hasira wakataka kuwaua mitume.
Injili
14Kisha watu walipoona ishara hii aliyoifanya walisema, “Kweli huyu ndiye yule nabii ajaye ulimwenguni.” 15Yesu alipotambua kuwa walikuwa wanataka kumkamata ili wamfanye kuwa mfalme wao, alijitenga, tena na akaenda mlimani yeye peke yake. 16Ilipokuwa jioni, wanafunzi wake walishuka kwenda ziwani. 17Wakapanda kwenye mtumbwi na walikuwa wakivuka kuelekea Kapernaumu. (Giza lilikuwa limeingia na Yesu alikuwa bado hajaja kwao). 18Wakati huo upepo mkali ulikuwa ukivuma, na bahari ilikuwa ikendelea kuchafuka. 19Tena wanafunzi wake walipokuwa wamepiga makasia kama ishirini na matano au thelathini, wakamwona Yesu akitembea juu ya bahari kuukaribia mtumbwi, na wakaogopa. 20Lakini akawambia, “Ni mimi! Msiogope.” 21Tena walikuwa tayari kumbeba kwenye mtumbwi, na mara mtumbwi ulifika kwenye nchi mahali walipokuwa wakienda. 22Siku iliyofuata, mkutano uliokuwa umesimama upande wa bahari waliona kuwa hakuna mtumbwi mwingine isipokuwa ule ambayo Yesu na wanafunzi wake walikuwa hawajaupanda lakini wanafunzi wake walikuwa wameenda zao wenyewe. 23(Ingawa, kulikuwa na baadhi ya mitumbwi iliyotoka Tiberia karibu na mahali walipokula mikate baada ya Bwana kutoa shukrani). 24Wakati makutano walipotambua kuwa sio Yesu wala wanafunzi wake walikuwa kule, wao wenyewe walipanda ndani ya mitumbwi wakaenda Kapernaumu wakimtafuta Yesu. 25Baada ya kumpata upande mwingine wa ziwa wakamuuliza, “Rabbi ulikuja lini huku?” 26Yesu akawajibu, akawambia, Amini, amini, mnanitafuta mimi, sio kwa sababu mliziona ishara, bali kwa sababu mlikula mikate na kushiba. 27Acheni kukifanyia kazi chakula chenye kuharibika, bali mkifanyie kazi chakula kidumucho hata milele kile ambacho mwana wa Adamu atawapa, kwa kuwa Mungu Baba ameweka muhuri juu yake.”
Watakatifu wa siku
- Kuhamishwa kwa masalia ya Wana wa Mfalme Waaminifu wa Urusi Boris na Gleb, walioitwa Romano na Daudi katika Ubatizo mtakatifu (1072 na 1115)
- Askofu Mtakatifu Athanasio, Patriarki wa Konstantinopoli, mtenda miujiza wa Lubny na wa Kharkiv (1654)
- Wafiadini Hespero na Zoe na watoto wao Kiriako na Theodulo (karne ya 2)
- Mfalme Mwaminifu Boris Sawa na Mitume, aliyeitwa Mikaeli katika Ubatizo mtakatifu (907), aliyebatizwa pamoja na watu wake katika karne ya 9 (Bulgaria)
- Ikoni ya Mama wa Mungu ya Putyvl (1635)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 2 Mei katika kalenda ya kanisa ni 15 Mei katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki