Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Mei 2027 › 3 Mei

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 3 Mei 2027

Jumatatu · Juma la 6 la Pasaka

Sikukuu na watakatifu

Watakatifu Filipo na Yakobo, mitume

Sikukuu · Rangi ya liturujia: nyekundu

Masomo ya siku

Somo la kwanza

1 Kor 15:1–8

1Sasa ninawakumbusha, akina kaka na akina dada, juu ya injili niliyowahubiria, ambayo mliipokea na kusimama kwayo. 2Ni katika injili hii mmeokolewa, kama mkilishika imara neno nililowahubiri ninyi, isipokuwa mliamini bure. 3Kama kwanza nilivyo ipokea kwa umuhimu niliileta kwenu kama ilivyo: kwamba kutokana na maandiko, Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, 4kutokana na maandiko alizikwa, na kwamba alifufuka siku ya tatu. 5Na kwamba alimtokea Kefa, kisha kwa wale kumi na wawili. 6Kisha aliwatokea kwa wakati mmoja akina kaka na akina dada zaidi ya mia tano. Wengi wao bado wako hai, lakini baadhi yao wamelala usingizi. 7Kisha alimtokea Yakobo, kisha mitume wote. 8Mwisho wa yote, alinitokea mimi, kama vile kwa mtoto aliye zaliwa katika wakati usio sahihi.

Wimbo wa katikati

Zab 19:1–4

1Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi. Mbingu za tangaza utukufu wa Mungu, na mawingu hufanya kazi ya mikono yake ijulikane! 2Siku hadi siku hotuba hutokea; usiku hadi usiku hufunua maarifa. 3Hakuna hotuba wala misemo; sauti zao hazisikiki. 4Bali maneno yao husambaa nje duniani kote, na hotuba zao hata mwisho wa dunia. Yeye ametengeneza hema kwa ajili ya jua kati yao.

Injili

Yn 14:6–14

6Yesu alimwambia, “ Mimi ndiye njia, kweli, na uzima; hakuna awezaye kuja kwa Baba isipokuwa kupitia kwangu. 7Kama mngeli nijua mimi, mngalikuwa mnamjua na Baba yangu pia; kuanzia sasa na kuendelea mnamjua na mmeshamuona yeye.” 8Philipo alimwambia Yesu, “Bwana, tuonyeshe Baba, na hivyo itakuwa imetutosha.” 9Yesu akamwambia, “Sijakuwa pamoja nanyi kwa muda mrefu, na bado hunijui mimi, Philipo? Yeyote aliyeniona mimi amemwona Baba; Jinsi gani unasema, 'Tuonyeshe Baba'? 10Hamuamini kuwa mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Maneno ninayoyasema kwenu sisemi kwa kusudi langu mwenyewe; badala yake, ni Baba anayeishi ndani yangu anayetenda kazi yake. 11Niamini mimi, kwamba niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani yangu; kadhalika niamini mimi kwa sababu ya kazi zangu hasa. 12Amini, amini, nawaambia, yeye aniaminiye, mimi kazi zile nizifanyazo, atazifanya kazi hizi pia; na atafanya hata kazi kubwa kwasababu ninakwenda kwa Baba. 13Chochote mkiomba katika jina langu, nitafanya ili kwamba Baba aweze kutukuzwa katika Mwana. 14Kama mkiomba kitu chochote katika jina langu, hilo nitafanya.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 3 Mei

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki