Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Machi 2027 › 5 Machi
Kalenda ya Kiorthodoksi · 20 Februari (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 5 Machi 2027
Ijumaa · Wiki ya Kuacha Nyama · Sauti ya 6
Sikukuu na watakatifu
Ijumaa ya Wiki ya Kuacha Nyama
Siku ya mfungo
Samaki wanaruhusiwa
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
1Kutoka kwa mzee kwenda kwa mwanamke mteule na watoto wake, ambao niwapendao katika kweli na si mimi tu, bali na wote wale wanao ifahamu kweli, 2kwa sababu ya kweli iliyomo ndani yetu na itakayodumu pamoja nasi milele. 3Neema, rehema, amani zitakuwa nasi kutoka kwa Mungu Baba na kutoka kwa Yesu Kristo, Mwana wa Baba, katika kweli na pendo. 4Ninafurahi sana kwamba nimegundua baadhi ya watoto wanaenenda katika kweli, kama vile tu tulivyoipokea amri hii kutoka kwa Baba. 5Na sasa nakusihi wewe, mwanamke, siyo kwamba nakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tokea mwanzo, kwamba tunapaswa kupendana sisi kwa sisi. Na huu ndiyo upendo, tunaopaswa kuenenda, kulingana na amri yake. 6Hii ndiyo ile amri, kama mlivyoisikia tokea mwanzo, kwamba mnapaswa kuenenda katika hiyo. 7Kwa kuwa wadanganyifu wengi wamesambaa katika ulimwengu, na hawakiri kwamba Yesu Kristo alikuja katika mwili. Huyu ndiye mdanganyifu na mpinga Kristo. 8Jiangalieni wenyewe kwamba hampotezi mambo yale tuliyokwisha fanyia kazi, lakini ili kwamba mweze kuipokea tuzo kamili. 9Yeyote aendeleae mbele na hadumu katika fundisho la Kristo, hana Mungu. Yeye adumuye katika fundisho anaye Baba na Mwana pia. 10Kama mtu anakuja kwenu na haleti fundisho hili, msimkaribishe katika nyumba zenu na msimsalimie. 11Kwa kuwa amsalimuye hushiriki katika matendo yake maovu. 12Ninayo mambo mengi ya kukuandikia, na sikutaka kuyaandika kwa karatasi na wino. Lakini natumaini kuja kwenu na kuongea uso kwa uso, kwamba furaha yetu ipate kufanywa kamili. 13Watoto wa dada yenu mteule wanawasalimia.
Injili
22Askari wakampeleka Yesu mahali paitwapo Goligotha (maana ya tafsiri hii ni, Sehemu ya Fuvu la kichwa). 25Yapata saa tatu asubuhi walipomsulibisha. 33Ilipofika saa sita, giza likaja juu ya nchi yote hadi saa tisa. 34Wakati wa saa tisa, Yesu alipiga kelele kwa sauti kubwa, “Eloi, Eloi, lama sabaktani?” ikiwa na maana “Mungu wangu, Mungu wangu, kwa nini umeniacha?” 35Baadhi ya hao waliosimama waliposikia wakasema, “Tazama, anamwita Eliya.” 36Mtu mmoja akakimbia, akajaza siki katika sponji na kuiweka juu ya mti wa mwanzi, akampa ili anywe. Mtu mmoja akasema, “Ngoja tuone kama Eliya atakuja kumshusha chini.” 37Kisha Yesu akalia kwa sauti kubwa na akafa. 38Pazia la hekalu likagawanyika vipande viwili toka juu mpaka chini. 39Ofisa mmoja aliyekuwa amesimama akimwelekea Yesu, alipoona amekufa kwa jinsi ile, akasema, “Kweli huyu mtu alikuwa Mwana wa Mungu.” 40Walikuwepo pia wanawake waliokuwa wakitazama kwa mbali. Miongoni mwao alikuwepo Mariamu Magdalena, Mariamu (mama yake Yakobo mdogo wa Yose), na Salome. 41Wakati alipokuwa Galilaya walimfuata na kumtumikia. Na wanawake wengine wengi pia waliambatana naye hadi Yerusalemu.
Watakatifu wa siku
- Mtakatifu Mtawa Leo, Askofu wa Katania (karibu 780)
- Watawa Wafiadini 34 wa Valaam: Tito, Tikhon, Gelasio, Sergio, Barlaamu, Sava, Kononi, Silvesta, Kiprian, Pimeni, Yohana, Samona, Yona, Daudi, Kornelio, Nifonti, Athanasio, Serapioni, Barlaamu, Athanasio, Antoni, Luka, Leontio, Tomaso, Dionisio, Filipo, Ignatio, Basili, Pakomio, Basili, Theofilo, Yohana, Theodoro, Yohana (1578)
- Mfiadini wa Kikasisi Nikolao, padri (1938)
- Mfiadini wa Kikasisi Sadoki (Shah-Dust), Askofu wa Uajemi, na pamoja naye wafiadini 128 (342-344)
- Mtakatifu Mtawa Agatho, Papa wa Roma (682)
- Mwana wa Mfalme Mwaminifu Yaroslav Mwenye Hekima (1054)
- Mtakatifu Mtawa Agatho wa Mapango ya Kyiv (karne ya 13-14)
- Mtawa Mfiadini Kornelio, abati wa Mapango ya Pskov (1570)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 20 Februari katika kalenda ya kanisa ni 5 Machi katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki