Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Februari 2027 › 3 Februari
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 3 Februari 2027
Jumatano · Juma la 4 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Jumatano ya Juma la 4 la Mwaka
Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani
Mt. Ansgari, askofu · Kumbukumbu ya hiari
Mt. Blasi, askofu na shahidi · Kumbukumbu ya hiari
Masomo ya siku
Somo la kwanza
4Hamjataabika au kuteseka mkishindana na dhambi kiasi cha kuishiwa damu. 5Tena mmesahau kule kutiwa moyo ambako kunawaelekeza kama watoto wa kiume: “Mwanangu, usiyachukuwe kwa wepesi marudia ya Bwana, wala usikate tamaa unapo rekebishwa na yeye.” 6Kwa kuwa Bwana humrudi yeyote ambaye anampenda, na humwadhibu kila mwana ambaye humpokea. 7Stahimili majaribu kama kurudiwa. Mungu hushughulika nanyi kama anavyoshughulika na watoto, maana ni mtoto yupi ambaye baba yake hawezi kumrudi? 11Hakuna adhabu inayofurahisha kwa wakati huo. Huwa na maumivu. Hata hivyo, baadaye huzaa tunda la amani ya utauwa kwa wale waliofundishwa nayo. 12Kwa hiyo inueni mikono yenu iliyolegea na kufanya magoti yenu yaliyo dhaifu kuwa yenye nguvu tena; 13nyosheni mapito ya nyayo zenu, ili kwamba yeyote aliye mlemavu hataongozwa upotevuni lakini apate kuponywa. 14Tafuteni amani na watu wote, na pia utakatifu ambao bila huo hakuna atakayemwona Bwana. 15Muwe waangalifu ili kwamba asiwepo atakayetengwa mbali na neema ya Mungu, na kwamba lisije shina la uchungu litakalochipuka na kusababisha shida na kukengeusha wengi.
Wimbo wa katikati
1Zaburi ya Daudi. Nitamsifu Yahwe maisha yangu yote, na vyote vilivyomo ndani yangu, nitalisifu jina lake takatifu. 2Maishani mwangu mwote nitamsifu Yahwe, na kukumbuka matendo yake yote mazuri. 13Kama vile baba alivyo na huruma kwa watoto wake, ndivyo Yahwe alivyo na huruma kwao wamchao. 14Maana anajua tulivyo umbwa; anajua kuwa tu mavumbi. 17Lakini agano la uaminifu wa Yahwe uko kwa wale wamchao yeye milele hata milele. Haki yake ni endelevu kwa uzao wao. 18Wanashika agano lake na kukumbuka kutii maagizo yake.
Injili
1Na akaondoka hapo na kwenda mjini kwao, na wanafunzi wake wakamfuata. 2Sabato ilipofika, alianza kufundisha katika Sinagogi. Watu wengi walimsikia na wakashangazwa. Wakasema, “Amepata wapi mafundisho haya?” “Ni hekima gani hii aliyopewa?” “Anatendaje miujiza hii kwa mikono yake?” 3“Je huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu na ndugu yao kina Yakobo, Yose, Yuda na Simioni? Je dada zake si wanaishi papa hapa pamoja nasi?” Na hawakufurahishwa na Yesu. 4Yesu akawaambia, “Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika mji wake na miongoni mwa ndugu zake na nyumbani mwake.” 5Hakuweza kutenda miujiza hapo, ila aliwawekea mikono wagonjwa wachache akawaponya. 6Alishangazwa sana kwa sababu ya kutokuamini kwao. Kisha alivitembelea vijiji vya jirani akifundisha.
Watakatifu wa siku
- Mt. Ansgari, askofu
- Mt. Blasi, askofu na shahidi
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki