Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Februari 2027 › 3 Februari

Kalenda ya Kiorthodoksi · 21 Januari (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 3 Februari 2027

Jumatano · Wiki ya 36 baada ya Pentekoste · Sauti ya 2

Sikukuu na watakatifu

Mtakatifu Mtawa Maksimo Mwungamaji (662)

Siku ya mfungo

Samaki wanaruhusiwa

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Waraka

Yak 1:1–18

1Yakobo, mtumwa wa Mungu na wa Bwana Yesu Kristo, kwa makabila kumi na mbili yaliyotawanyika, salaam. 2Hesabuni kuwa ni furaha zaidi, ndugu zangu, mnapopita katika matatizo mbali mbali, 3mkijua kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huwapa uvumilivu. 4Acheni uvumilivu uikamilishe kazi yake, kwamba muweze kukomaa kikamilifu, bila kupungukiwa katika lolote. 5Lakini kama mtu kati yenu anahitaji hekima, aiombe kutoka kwa Mungu, ambaye hutoa kwa ukarimu na pasipo kukemea kwa wote wamwombao, na atawapa hekima. 6Lakini omba kwa imani, bila shaka, kwa kuwa mwenye kutia shaka ni kama mawimbi katika bahari, huchukuliwa na upepo na kutupwa huku na huko. 7Kwa hakika mtu huyu asifikirie kwamba atapokelewa ombi lake kutoka kwa Bwana; 8mtu huyu ana nia mbili, si imara katika njia zake zote. 9Ndugu maskini anapaswa kujivuna katika kusimama kwake juu, 10wakati huo huo ndugu tajiri katika unyenyekevu wake, kwa sababu atatoweka kama ua la kondeni katika shamba analopita. 11Jua huchomoza na joto la kuunguza kukausha mimea, na maua huanguka na uzuri wake hufa. Vivyo hivyo watu matajiri watachakaa katikati ya kazi zao. 12Amebarikiwa mtu yule anayevumilia majaribu, kwa kuwa baada ya kushinda jaribu hilo, atapokea taji ya uzima, ambayo imeahidiwa kwa wale wampendao Mungu. 13Mtu yeyote hapaswi kusema anapojaribiwa, “Jaribu hili linatoka kwa Mungu,” kwa sababu Mungu hajaribiwi na uovu, na Mungu mwenyewe hamjaribu yeyote. 14Kila mtu hujaribiwa na tamaa zake mbaya zinazomshawishi na kumvuta mbali. 15Ndipo baada ya tamaa ya dhambi kubeba mimba, dhambi huzaliwa, na baada ya dhambi kukomaa sawasawa, huishia katika mauti. 16Ndugu zangu wapendwa, msidanganyike. 17Kila zawadi iliyo nzuri na kila zawadi iliyokamilika hutoka juu, hushuka chini kutoka kwa Baba wa nuru. Kamwe habadiliki kama kivuli kibadilikavyo. 18Mungu alichagua kutupa sisi uzima kwa Neno la kweli, ili kwamba tuweze kuwa kama uzao wa kwanza miongoni mwa viumbe vyake.

Injili

Mk 10:11–16

11Akawaambia, “Yeyote amwachaye mke wake na kumwoa mwanamke mwingine, anafanya uzinzi dhidi yake. 12Mwanamke naye akimwacha mme wake na kuolewa na mwanamme mwingine, anafanya uzinzi.” 13Nao walimletea watoto wao wadogo ili awaguse, lakini wanafunzi wakawakemea. 14Lakini Yesu alipotambua hilo, hakufurahishwa nalo kabisa akawaambia, “Waruhusuni watoto wadogo waje kwangu, na msiwazuie, kwa sababu walio kama hawa ufalme wa Mungu ni wao. 15Ukweli nawaambia, yeyote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hakika hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu. 16Kisha akawachukua watoto mikononi mwake na akawabariki akiwawekea mikono yake juu yao.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 3 Februari

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 21 Januari katika kalenda ya kanisa ni 3 Februari katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki