Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Januari 2027 › 16 Januari
Kalenda ya Kiorthodoksi · 3 Januari (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 16 Januari 2027
Jumamosi · Wiki ya 33 baada ya Pentekoste · Sauti ya 7
Sikukuu na watakatifu
Jumamosi kabla ya Theofania
Siku za Noeli (Sviatki)
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka (Jumamosi kabla ya Theofania)
14Ninaandika mambo haya kwako, na ninatumaini kuja kwako hivi karibuni. 15Lakini ikiwa nitachelewa, ninaandika ili upate kujua namna ya kuenenda katika nyumba ya Mungu, ambalo ni kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msaada wa kweli. 16Na haipingiki kwamba kweli ya Uungu uliyofunuliwa ni mkuu: “Alionekana katika mwili, akathibitishwa na Roho, akaonekana na malaika, akatangazwa miongoni mwa mataifa, akaaminiwa na ulimwengu, na akachukuliwa juu katika utukufu.” 4:1Sasa Roho anasema waziwazi kwamba katika nyakati zijazo baadhi ya watu wataiacha imani na kuwa makini kusikiliza roho zidanganyazo na mafundisho ya kipepo yatakayofundishwa 2katika uongo na unafiki. Dhamiri zao zitabadilishwa. 3Watawazuia kuoa na kupokea vyakula ambavyo Mungu aliviumba vitumiwe kwa shukrani miongoni mwao waaminio na wenye kuijua kweli. 4Kwa sababu kila kitu ambacho Mungu amekiumba ni chema. Hakuna ambacho tunapokea kwa shukrani kinastahili kukataliwa. 5Kwa sababu kinatakaswa kupitia neno la Mungu na kwa njia ya maombi.
Injili (Jumamosi kabla ya Theofania)
1Katika siku zile Yohana Mbatizaji alikuja akihubiri katika nyika ya Yuda akisema, 2“Tubuni kwa maana ufalme wa mbinguni u karibu.” 3Kwa maana huyu ndiye aliyenenwa na nabii Isaya akisema, “sauti ya mtu aitaye kutoka jangwani; 'wekeni tayari njia ya Bwana, yanyoosheni mapito yake.”' 4Sasa Yohana alivaa manyoya ya ngamia na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni. 5Kisha Yerusalemu, Yuda yote, na eneo lote linalozunguka mto Yorodani wakaenda kwake. 6Walikuwa wakibatizwa naye katika mto Yorodani huku wakitubu dhambi zao. 7Lakini alipowaona wengi wa mafarisayo na masadukayo wakija kwake kubatizwa, akawaambia, ''Enyi uzao wa nyoka wenye sumu nani aliye waonya kuikimbia ghadhabu inayokuja? 8Zaeni matunda yaipasayo toba. 9Na msifikiri na kusemezana miongoni mwenu, 'Tunaye Ibrahimu kama baba yetu.' Kwa kuwa nawaambieni Mungu anaweza kumwinulia Ibrahimu watoto hata kutoka katika mawe haya. 10Tayari shoka limekwisha kuwekwa kwenye mzizi wa miti. Kwahiyo kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa kwenye moto. 11Ninawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba. Lakini yeye ajaye baada yangu ni mkuu kuliko mimi nami sistahili hata kubeba viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
Watakatifu wa siku
- Kabla ya Sikukuu ya Epifania
- Nabii Malaki (karibu 400 K.K.)
- Mfiadini Gordio (karne ya 4)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 3 Januari katika kalenda ya kanisa ni 16 Januari katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki