Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Januari 2027 › 8 Januari

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 8 Januari 2027

Ijumaa · Kipindi cha Noeli

Sikukuu na watakatifu

Ijumaa baada ya Epifania

Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: nyeupe

Kufunga na toba

Siku ya toba

Kila Ijumaa ni siku ya toba; kila baraza la maaskofu huamua jinsi inavyoadhimishwa: kujinyima nyama au tendo lingine la toba. Kufunga kunawahusu wenye miaka 18 hadi 59, kujinyima nyama kuanzia miaka 14.

Masomo ya siku

Somo la kwanza

1 Yoh 4:7–10

7Wapendwa, tupendane sisi kwa sisi, kwa vile upendo ni wa Mungu, na kila mmoja apendaye amezaliwa na Mungu na kumjua Mungu. 8Yeye asiyependa hamjui Mungu, kwa sababu Mungu ni upendo. 9Katika hili pendo la Mungu lilifunuliwa miongoni mwetu, kwamba Mungu alimtuma Mwanae wa pekee ulimwenguni ili tuishi kupitia yeye. 10Katika hili pendo, si kwamba tulimpenda Mungu, lakini yeye alitupenda, na akamtuma Mwanawe awe fidia ya dhambi zetu.

Wimbo wa katikati

Zab 72:1–4, 7–8

1Zaburi ya Sulemani. Mpe mfalme amri ya haki yako, Mungu, haki yako kwa wana wa mfalme. 2Naye awaamue watu wako kwa haki na maskini wako kwa haki sawa. 3Milima iwazalie watu amani; vilima navyo vizae haki. 4Naye awahukumu watu maskini; awaokoe watoto wa wahitaji na kuwavunja vipande vipande wenye kuwatesa. 7Mwenye haki na astawi kwa wakati wake, na amani iwepo kwa wingi mpaka mwezi utakapotoweka. 8Na awe na mamlaka toka bahari na bahari, na kutoka Mto hadi miisho ya dunia.

Injili

Mk 6:34–44

34Walipofika pwani, aliona umati mkubwa na akawahurumia, kwa sababu walikuwa kama kondoo wasiokuwa na mchungaji. Na akaanza kuwafundisha mambo mengi. 35Muda ulipoendelea sana, wanafunzi wakamjia wakamwambia,”Hapa ni mahali pa faragha na muda umeendelea. 36Uwaage waende miji ya jirani na vijiji ili wakajinunulie chakula.” 37Lakini akawajibu akisema, “Wapeni ninyi chakula.” Wakamwambia, “Tunaweza kwenda na kununua mikate yenye thamani ya dinari mia mbili na kuwapa wale?” 38Akawambia,” Mna mikate mingapi? Nendeni mkaangalie.” walipopata wakamwambia, “Mikate mitano na samaki wawili.” 39Akawaamuru watu waketi katika makundi juu ya majani mabichi. 40Wakawaketisha katika makundi; makundi ya mamia kwa hamsini. 41Kisha akachukua mikate mitano na samaki wawili, na kutazama mbinguni, akaibariki kisha akawapa wanafunzi waweke mbele ya umati. Na kisha aligawa samaki wawili kwa watu wote. 42Walikula wote hadi wakatosheka. 43Walikusanya vipande vya mikate iliyobaki, Vikajaa vikapu kumi na viwili, na pia vipande vya samaki. 44Na walikuwa wanaume elfu tano waliokula mikate.

Watakatifu wa 8 Januari

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki