Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Januari 2027 › 5 Januari
Kalenda ya Kiorthodoksi · 23 Desemba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 5 Januari 2027
Jumanne · Wiki ya 32 baada ya Pentekoste · Sauti ya 6
Sikukuu na watakatifu
Kabla ya Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Kristo
Mfungo wa Kuzaliwa kwa Bwana
Mfungo: chakula kilichopikwa bila mafuta
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
1Ndugu zangu, siyo wengi wenu mnapaswa kuwa walimu, mkijua kwamba tutapokea hukumu kubwa zaidi. 2Kwa kuwa wote tunakosea katika njia nyingi. Kama yeyote huwa hajikwai katika maneno yake, huyo ni mtu mkamilifu, aweza kudhibiti mwili wake wote pia. 3Sasa kama tunaweka lijamu za farasi katika vinywa vyao wanatutii, na tunaweza kuigeuza miili yao yote. 4Tambua pia kwamba meli, ingawa ni kubwa na husukumwa na upepo mkali, zinaongozwa kwa usukani mdogo sana kwenda popote anakotaka nahodha. 5Vivyo hivyo, ulimi ni kiungo kidogo cha mwili, lakini hujisifia makuu sana. Angalia msitu mkubwa unavyoweza kuwashwa kwa cheche ndogo ya moto! 6Ulimi pia ni moto, ni ulimwengu wa uovu, umewekwa miongoni mwa viungo vya mwili wetu, ambao hunajisi mwili wote na huiweka juu ya moto njia ya maisha, na wenyewe kuchomwa moto wa kuzimu. 7Kila aina ya mnyama wa polini, ndege, kitambaacho na kiumbe cha baharini kinadhibitiwa na wanadamu. 8lakini hakuna mwanadamu hata mmoja ambaye anaweza kudhibiti ulimi; ni uovu usiotulia, umejaa sumu ya kufisha. 9Kwa ulimi twamtukuza Bwana na Baba yetu, na kwa huo twawalaani watu ambao wameumbwa kwa mfano wa Mungu. 10Katika kinywa hichohicho husema maneno ya baraka na laana. Ndugu zangu mambo haya hayapaswi kuwa.
Injili
2Na Mafarisayo walikuja kumjaribu na wakamuuliza, “Ni halali kwa mwanamume kuachana na mke wake?” 3Yesu akawajibu, “Musa aliwaamuru nini?” 4Wakasema, “Musa aliruhusu kuandika cheti cha kuachana na kisha kumfukuza mwanamke.” 5“Ni kwa sababu ya mioyo yenu migumu ndiyo maana aliwaandikia sheria hii,” Yesu aliwaambia. 6“Lakini kutoka mwanzo wa uumbaji, 'Mungu aliwaumba mwanamume na mwanamke.' 7Kwa sababu hii mwanamume atamwacha baba yake na mama yake na ataungana na mke wake, 8na hao wawili watakuwa mwili mmoja; Kwa kuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. 9Kwa hiyo alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.” 10Walipokuwa ndani ya nyumba, wanafunzi wake wakamwuliza tena kuhusu hili. 11Akawaambia, “Yeyote amwachaye mke wake na kumwoa mwanamke mwingine, anafanya uzinzi dhidi yake. 12Mwanamke naye akimwacha mme wake na kuolewa na mwanamme mwingine, anafanya uzinzi.”
Watakatifu wa siku
- Wafiadini wa Krete: Theodulo, Saturnino, Euporo, Gelasio, Eunikiano, Zotiko, Pompio, Agathopodo, Basilide na Eugaresto (karne ya 3)
- Mfiadini wa Kikasisi Basili, padri, na Watawa Wafiadini Makario na Yohana (1938)
- Mtakatifu Mtawa Nifonti, Askofu wa Kipro (karne ya 4)
- Mtakatifu Mtawa Paulo, Askofu wa Neokaisaria (karne ya 4)
- Askofu Mtakatifu Theoktisto, Askofu Mkuu wa Novgorod (1310)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 23 Desemba katika kalenda ya kanisa ni 5 Januari katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki