Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Desemba 2026 › 6 Desemba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 6 Desemba 2026
Jumapili · Juma la 2 la Majilio
Sikukuu na watakatifu
Dominika ya 2 ya Majilio
Dominika · Rangi ya liturujia: zambarau
Masomo ya siku
Somo la kwanza
1''Faraja, faraja watu wangu,'' amesema Mungu. 2''Ongea kwa upole kwa Yerusalemu; na tangaza vita vimeisha, maana maovu yao yamesamehewa, maana alipokea mara mbili kutoka kwa mkono wa Yahwe kwa dhambi zao.'' 3Sauti inalia nje, ''Katika jangwa tengeneza njia ya Yahwe; njoosha njia ya Araba katika njia kuu ya Mungu.'' 4Kila bonde litanyanyuliwa juu, kila mlima na kilima kitasawazishwa; na aridhi ya mwinuko itasawazishwa, mahali palipokwaruzwa patakuwa na usawa; 5na utukufu wa Mungu utafunuliwa, na watu wote wataona kwa pamoja; maana mdomo wa Yahwe umezungumza. 9Nenda juu ya mlima mrefu, Sayuni, mbeba taarifa njema. waambie miji ya Yuda, ''Hapa ni Mungu wako!'' 10Angalia, Bwana Yahwe anakuja kama mpiganaji shujaa na jeshi imara linatawa juu yake. Ona, zawadi yako iko kwake, na wale walikombolewa wataenda mbele yake. 11Atalilisha kundi lake kama mchungaji, Atawakusanya kondoo katika jeshi lake, na kulichukua karibu na moyo wake, kwa upole atawongoza wake kuwauuguza watoto wao.
Wimbo wa katikati
8Nitasikiliza yale Yahwe Mungu asemayo, maana yeye atafanya amani pamoja na watu wake, wafuasi wake waminifu. Lakini lazima wasirudi tena katika njia za kipumbavu. 9Hakika wokovu wake u karibu na wale wanao mwabudu yeye; kisha utukufu utabaki katika nchi yetu. 10Uaminifu wa agano na uaminifu vimekutana pamoja; haki na amani vimebusiana. 11Uaminifu unatoa chemchem kutoka ardhini, na haki hutazama chini kutoka mawinguni. 12Ndiyo, Yahwe atatoa baraka zake njema, na nchi itatoa mazao yake. 13Haki itaenda mbele zake na kufanya njia kwa ajili ya nyayo zake.
Somo la pili
8Hii haiwezi kuchenga ujumbe wako, wapendwa, kwamba siku moja kwa bwana ni kama miaka elfu moja. Na miaka elfu moja ni kama siku moja. 9Si kwamba Bwana anafanya pole pole kutimiza ahadi, kama inavyofikiriwa kuwa, Lakini yeye ni mvumilivu kwa ajili yenu, yeye hatamani hata mmoja aangamie, Lakini hutamani kutoa muda ili wote wapate kutubu. 10Ingawa, siku ya Bwana itakuja kama mwizi, mbingu itapita kwa kupaza kelele. Vitu vitateketezwa kwa moto. Nchi na vitu vyote vilivyomo vitafunuliwa wazi. 11Kwa kuwa vitu vyote vutateketezwa kwa njia hii. Je utakuwa mtu wa aina gani? Uishi kitakatifu na maisha ya kimungu. 12Inakupasa kujua na kutambua haraka ujio wa siku ya Mungu. Siku hiyo mbingu itateketezwa kwa moto. Na vitu vitayeyushwa katika joto kali. 13Lakini kutokana na ahadi yake, tunasubiri mbingu mpya na nchi mpya, ambapo wenye haki wataishi 14Hivyo wapendwa kwa kuwa tunatarajia vitu hivi, jitahidi kuwa makini na kutolaumika na kuwa na amani pamoja naye.
Injili
1Huu ni mwanzo wa injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. 2Kama ilivyoandikwa na nabii Isaya, “Tazama, ninamtuma mjumbe wangu mbele yako, mmoja atakayetayarisha njia yako. 3Sauti ya mtu aitaye nyikani, “Ikamilisheni njia ya Bwana; zinyosheni njia zake”. 4Yohana alikuja, akibatiza nyikani na kuhubiri ubatizo wa toba kwa msamaha wa dhambi. 5Nchi yote ya Yudea na watu wote wa Yerusalemu walikwenda kwake. Walikuwa wakibatizwa naye katika mto Yordani, wakiungama dhambi zao. 6Yohana alikuwa anavaa vazi la manyoya ya ngamia na mkanda wa ngozi kiunoni mwake, na alikuwa anakula nzige na asali ya porini. 7Alihubiri na kusema, “Yupo mmoja anakuja baada yangu mwenye nguvu zaidi kuliko mimi, na sina hadhi hata ya kuinama chini na kufungua kamba za viatu vyake. 8Mimi niliwabatiza kwa maji, lakini yeye atawabatiza ninyi kwa Roho Mtakatifu.”
Watakatifu wa siku
- Mt. Nikolao, askofu
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki