Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Desemba 2026 › 3 Desemba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 3 Desemba 2026
Alhamisi · Juma la 1 la Majilio
Sikukuu na watakatifu
Alhamisi ya Juma la 1 la Majilio
Kumbukumbu · Rangi ya liturujia: nyeupe
Mt. Fransisko Ksaveri, padre · Kumbukumbu
Masomo ya siku
Somo la kwanza
1Siku hiyo wimbo huu utaimbwa katika nchi ya Yuda: Tuna mji imara; Mungu amefanya wokovu katika kuta na ngome zake. 2Fungua lango, ili mataifa yenye haki yaweze na yenye kutunza imani yaweze kuingia ndani. 3Akili mlionayo, mtamuhifadhi yeye katika amani kamili, maana anawamini ninyi. 4Mwamini Yahwe daima; maana Yaha, Yahwe, ni mwamba wa milele. 5Maana atawashusha wale wote wenye kiburi; mji ulio juu atushusha chini, ataushusha chini kwenye aridhi; na ataulinganisha na mavumbi. 6Utakanyagwakanyagwa chini na miguu ya walio masikini na wahitaji.
Wimbo wa katikati
1Mshukuruni Yahwe, kwa kuwa ni mwema, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele. 8Ni bora kuwa na makazi katika Yahwe kuliko kumtumainia mwanadamu. 9Ni bora kukimbilia katika Yahwe kuliko kuamini katika wakuu. 19Unifungulie milango ya haki; nitaingia na nitamshukuru Yahwe. 20Hili ni lango la Yahwe; wenye haki hupitia kwalo. 21Nitakushukuru wewe, kwa kuwa ulinijibu, na umekuwa wokovu wangu. 25Tafadhali, Yahwe, utupe ushindi! Tafadhali, Yahwe, utupe mafanikio! 26Amebarikiwa yule ajaye katika jina la Yahwe; tunakubariki kutoka katika nyumba ya Yahwe. 27Yahwe ni Mungu, na ametupa sisi nuru; ifungeni dhabihu kwa kamba pembeni mwa madhabahu.
Injili
21Si kila mtu aniambiaye mimi, 'Bwana, Bwana,' ataingia katika ufalme wa mbinguni, bali ni yule pekee atendaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 24Kwa hiyo, kila mmoja asikiaye maneno yangu na kutii atafanana na mtu mwenye hekima aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba. 25Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, na upepo ukaja na ukaipiga nyumba hiyo, lakini haikuweza kuanguka chini, kwa kuwa ilikuwa imejengwa juu ya mwamba. 26Lakini kila mtu anayesikia neno langu na asilitii, atafananishwa na mtu mpumbavu aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga. 27Mvua ikaja, mafuriko yakaja, na upepo ukaja na kuipiga nyumba hiyo. Na ikaanguka, na uharibifu wake ukakamilika.”
Watakatifu wa siku
- Mt. Fransisko Ksaveri, padre
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki