Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2026 › 8 Novemba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 8 Novemba 2026

Jumapili · Juma la 32 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Dominika ya 32 ya Mwaka

Dominika · Rangi ya liturujia: kijani

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Haimo katika tafsiri hii

Wimbo wa katikati

Zab 63:1–7

1Zaburi ya Daudi, wakati yeye alipokuwa katika jangwa la Yuda. Mungu, wewe ni Mungu wangu! Ninakutafuta wewe kwa bidii, moyo wangu unakiu yako, mwili wangu unakutamani sana wewe, katika ukame na nchi iliyochoka mahali ambapo hakuna maji. 2Hivyo nimekutafuta wewe katika watu watakatifu kuona nguvu zako na utukufu wako. 3Kwa sababu uaminifu wa agano lako ni bora kuliko uhai, midomo yangu itakusifu wewe. 4Hivyo nitakutukuza wewe niwapo hai; kwa jina lako nitainua mikono yangu juu. 5Itakuwa kana kwamba nilikula mlo wa mafuta na wenye kunona, kwa midomo ya furaha kinywa changu kitakusifu wewe, 6nikufikiripo kitandani mwangu na kukutafakari wewe wakati wa saa za usiku. 7Kwa maana umekuwa msaada wangu, na katika uvuli wa mbawa zako ninafurahia.

Somo la pili

1 The 4:13–18

13Hatutaki ninyi muelewe isivyo sahihi, enyi ndugu, juu ya hao waliolala, ili msije mkahuzunika kama wengine wasio na uhakika kuhusu wakati ujao. 14Iwapo tunaamini kuwa Yesu alikufa na akafufuka tena, vivyo hivyo Mungu atawaleta pamoja na Yesu hao waliolala mauti katika yeye. 15Kwa ajili ya hayo twawaambia ninyi kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaokuwepo wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wale waliolala mauti. 16Kwa kuwa Bwana mwenyewe atashuka toka mawinguni. Atakuja na sauti kuu, pamoja na sauti ya malaika mkuu, pamoja na parapanda ya Mungu, nao waliokufa katika Kristo watafufuka kwanza. 17Kisha sisi tulio hai, tuliobaki, tutaungana katika mawingu pamoja nao kumlaki Bwana hewani. Kwa njia hii tutakuwa na Bwana siku zote. 18Kwa hiyo, mfarijiane ninyi kwa ninyi kwa maneno haya.

Injili

Mt 25:1–13

1Ndipo ufalme wa mbinguni utafananishwa na wanawali kumi waliochukua taa zao na kuondoka kwenda kumpokea bwana harusi. 2Watano miongoni mwao walikuwa wapumbavu na watano wengine walikuwa werevu. 3Wanawali wapumbavu walipochukua taa zao, hawakuchukua mafuta yoyote. 4Bali wanawali welevu walichukua vyombo vyenye mafuta pamoja na taa zao. 5Sasa wakati bwana harusi amechelewa kufika, wote walishikwa usingizi na wakalala. 6Lakini wakati wa usiku wa manane kulikuwa na yowe, 'Tazama, bwana harusi! Tokeni nje mkampokee.' 7Ndipo hao wanawali waliamka wote na kuwasha taa zao. 8Wale wapumbavu waliwaambia wale welevu, 'Mtupatie sehemu ya mafuta yenu kwa sababu taa zetu zinazimika.' 9Lakini wale welevu waliwajibu na kuwaambia, 'Kwa kuwa hayatatutosha sisi na ninyi, badala yake nendeni kwa wanaouza mjinunulie kiasi kwa ajili yenu.' 10Wakati wameenda huko kununua, Bwana harusi alifika, na wote waliokuwa tayari walienda naye kwenye sherehe ya harusi, na mlango ulifungwa. 11Baadaye wale wanawali wengine pia walifika na kusema, 'Bwana, bwana, tufungulie.' 12Lakini alijibu na kusema, 'Kweli nawaambia, Mimi siwajui.' 13Kwa hiyo angalieni, kwa kuwa hamjui siku au saa.

Watakatifu wa 8 Novemba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili A, mwaka wa siku za kazi II.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki