Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2026 › 29 Oktoba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 16 Oktoba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 29 Oktoba 2026
Alhamisi · Wiki ya 22 baada ya Pentekoste · Sauti ya 4
Sikukuu na watakatifu
Mfiadini Longino, akida, aliyesimama karibu na Msalaba wa Bwana (karne ya 1)
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
2Endeleeni kuwa thabiti katika maombi. Kaeni macho katika hilo kwa shukrani. 3Ombeni pamoja kwa ajili yetu pia, ili kwamba Mungu afungue mlango kwa ajili ya neno, kunena siri ya ukweli ya Kristo. Kwa sababu ya hili nimefungwa minyororo. 4Na ombeni kwamba niweze kuliweka wazi, kama inavyonipasa kusema. 5Enenda kwa hekima kwa wale walioko nje, na muukomboe wakati. 6Maneno yenu na yawe na neema wakati wote, na yakolee chumvi majira yote, ili kwamba mweze kujua jinsi inavyowapasa kumjibu kila mtu. 7Kwa mambo yanayonihusu mimi, Tikiko atayafanya yajulikane kwenu. Yeye ni ndugu mpendwa, mtumishi mwaminifu, na mtumwa mwenzetu katika Bwana. 8Namtuma kwenu kwa ajili ya hili, kwamba mweze kujua mambo kuhusu sisi na pia kwamba aweze kuwatia moyo. 9Namtuma pamoja na Onesimo, ndugu yetu mpendwa mwaminifu, na mmoja wenu. Watawaambia kila kitu kilichotokea hapa.
Injili
7Sasa Herode, mtawala, alisikia yote yaliyo kuwa yakitokea alitaabika sana, kwa sababuu ilisemekana na baadhi kwamba Yohana mbatizaji amefufuka kutoka wafu, 8na baathi kwamba Elia amekwisha tokea, na kwa wengine kwamba mmoja wa manabii wa zamani amefufuka katika wafu tena. 9Herode alisema, “nilimchinja Yohana, lakini huyu ni nani ninae sikia habari zake? Na Herode alitafuta njia ya kumwona Yesu. 10Wakati waliporudi wale waliotumwa, wakamwamwambia kila kitu walicho fanya. Akawachukua pamoja naye, akaenda peke yake katika mji uitwao Bethsadia. 11Lakini makutano wakasikia kuhusu hili wakamfuata, na aliwakaribisha, na akaongea nao kuhusu ufalme wa Mungu, na aliwaponya wale waliohitaji uponyaji.
Injili (Mt. Longino, akida)
33Walipofika mahali paitwapo Galigotha, maana yake, “Eneo la fuvu la Kichwa.” 34Walimpa siki iliyochanganywa na nyongo anywe. Lakini alipoionja, hakuweza kuinywa. 35Wakati walipokuwa wamemsulibisha, waligawana mavazi yake kwa kupiga kura. 36Na waliketi na kumwangalia. 37Juu ya kichwa chake waliweka mashitaka dhidi yake yakisomeka, “Huyu ni Yesu, mfalme wa Wayahudi.” 38Wanyang'anyi wawili walisulibiwa pamoja naye, mmoja upande wa kulia wake na mwingine wa kushoto. 39Wale waliokuwa wakipita walimdhihaki, wakitikisa vichwa vyao 40na kusema, “Wewe uliyekuwa unataka kuliharibu hekalu na kulijenga katika siku tatu, jiokoe mwenyewe! Kama ni Mwana wa Mungu, shuka chini utoke msalabani!” 41Katika hali ile ile wakuu wa makuhani walikuwa wakimkashifu, pamoja na waandishi na wazee, na kusema, 42“Aliokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa mwenyewe. Yeye ni Mfalme wa Wayahudi. Na ashuke chini toka msalabani, ndipo tutakapomwamini. 43Alimtumaini Mungu. Acha Mungu amwokoe sasa kama anataka, kwa sababu alisema, 'Mimi ni Mwana wa Mungu.'” 44Na wale wanyang'anyi waliokuwa wamesulibiwa pamoja naye pia walisema maneno ya kumdhihaki. 45Sasa kutoka saa sita kulikuwa na giza katika nchi yote hadi saa tisa. 46Ilipofika saa tisa, Yesu akalia kwa sauti kuu, “Eloi, Eloi, lama thabakithan?” akimaanisha, “Mungu wangu, Mungu wangu, kwa nini umeniacha?” 47Wakati huo baadhi yao waliokuwa wamesimama pale walisikia, wakasema, “Anamwita Eliya.” 48Mara moja mmoja wao alikimbia kuchukua sifongo na kuijaza kinywaji kichungu, akaiweka juu ya mti na kumpa apate kunywa. 49Nao waliosalia wakasema, “Mwacheni peke yake, acheni tuone kama Eliya atakuja kumwokoa.” 50Kisha Yesu akalia tena kwa sauti kuu na akaitoa roho yake. 51Tazama, Pazia la hekalu lilipasuka sehemu mbili kutokea juu hadi chini. Na ardhi ikatetemeka na miamba ikapasuka vipande. 52Makaburi yalifunguka, na miili ya watakatifu wengi waliokuwa wamelala usingizi walifufuliwa. 53Walitoka kwenye makaburi baada ya ufufuo wake, waliingia mji mtakatifu, na wakaonekana na wengi. 54Basi yule akida na wale ambao walikuwa wakimtazama Yesu waliona tetemeko na mambo yaliyokuwa yakitokea, walijawa na woga sana na kusema, “Kweli huyu alikuwa Mwana wa Mungu.”
Watakatifu wa siku
- Mtakatifu Georgi Mwungamaji, padri (1931)
- Mfiadini wa Kikasisi Eugenio, padri (1937)
- Mfiadini wa Kikasisi Aleksi, padri (1938)
- Mfiadini wa Kikasisi Yohana, padri (1942)
- Mtakatifu Mtawa Longino, mlinzi wa lango wa Mapango ya Kyiv (karne ya 13-14)
- Mtakatifu Mtawa Longino wa Yarenga (1544-1545)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 16 Oktoba katika kalenda ya kanisa ni 29 Oktoba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki