Gundua › Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando › Sulemani
Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando · Sulemani
Farasi na utajiri wa Sulemani
1 Fal 10:26–29 · 2 Nya 1:14–17
1 Fal 10:26–2926Sulemani alikusanya pamoja magari n a wapanda farasi. Alikuwa na magari 1,400 na wapanda farasi elfu kumi na mbili ambao alikuwa amewaweka kwenye miji ya magari pamoja naye Yerusalemu.
27Mfalme alikuwa na fedha kule Yerusalemu, pamoja na mawe ardhini. Alitengeneza miti ya mierezi kuwa mingi kama mikuyu iliyo katika nyanda za chini.
28Sulemani alimiliiki farasi waliokuwa wamenunuliwa kutoka Misri na Kilikia. Wachuuzi wa mfalme waliwanunua kwa makundi, kila kundi kwa bei yake.
29Magari yalinunuliwa kutoka Misri kwa shekeli mia sita za fedha kila moja, na farasi kwa shekeli 150 kila moja. Vitu vingi katika hivi baadaye viliuzwa kwa wafalme wote wa Wahiti na Aramu.
2 Nya 1:14–1714Selemani akakusanya magari na wanaume waendesha farasi, naye alikuwa na magari 1,400 na waendesha farasi kumi na mbili elfu ambao aliwaweka katika miji ya magari, pamoja naye, mfalme katika Yerusalemu.
15Mfalme akatengeneza fedha na dhahabu kuwa vitu vya kawaida kama mawe katika Yerusalemu, na mbao za mierezi kuwa kama miti ya mikuyu iliyomo katika nyanda za chini.
16Selemani katika uagizaji wa farasi kutoka Misiri, wafanya biashara wake walinunua farasi kutoka Misiri kwa bei stahiki.
17Waliagiza gari kutoka Misiri kwa shekeli mia sita za fedha, na farasi mmoja kwa shekeli 150. Pia walinunua kutoka kwa wafalme wa Wahiti na wafalme wa Washamu.
Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.
Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY