Bible Explorer

Gundua › Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando › Wafalme wa Yuda

Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando · Wafalme wa Yuda

Amazia mfalme wa Yuda

2 Fal 14:1–20 · 2 Nya 25:1–28

2 Wafalme

2 Fal 14:1–20

1Katika mwaka wa pili wa Yehoashi mwana wa Yehoazi, mfalme wa Israeli, Amazia mwana wa Yoashi, mfalme wa Yuda, alianza kutawala.

2Alikuwa na umri wa miaka ishirini na tanao wakati alipoanza kutawala; alitawala kwa mda wa miaka ishirini na tisa katika Yerusalemu.

3Mama yake alikuwa anaitwa Yehoyadani, wa Yerusalemu. Alifanya yale yaliyo mema usoni mwa macho ya Yahwe, sio kama baba yake Daudi. Alifanya kila kitu ambacho Yoashi, baba yake, alichukuwa amekifanya.

4Lakini sehemu ya juu haikuondolewa. Watu wakaendelea kutoa dhabihu na kufukiza ubani katika sehemu mahala pa juu.

5Ikawa mara utawala wake ulipokuwa imara, aliwaua watumishi ambao waliokuwa wamemuua baba yake, mfalme.

6Ila hakuwaweka watoto wa wale wauaji kwenye kifo; isipokuwa, alifanya kutokana na kile kilichokuwa kimeandikwa kwenye sheria, kwenye kitabu cha Musa, kama Yahwe alivyokuwa ameamuru, akisema, “Wababa wasife kwa ajili ya watoto wao, wala watoto wasife kwa ajili ya makosa ya wazazi wao. Isipokuwa, kila mtu atakufa kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe.”

7Aliua maaskari elfu kumi wa Edomi kwenye bonde la chumvi; pia alimchukua Sela kwenye vita na kuiita Yoktheeli, ndivyo paitwavyo hadi leo.

8Kisha Amazia akatuma wajumbe kwa Yehoashi mwana wa Yehoahazi mwana wa Yehu mfalme wa Israeli, akisema, “Njoo, tuonane kila mmoja macho kwa macho kwenye mashinadano.”

9Lakini Yehoashi mfalme wa Israeli akawatuma wajumbe kurudi kwa Amazia mfalme wa Yuda, akisema, “Mbaruti uliokuwa Lebanoni ulituma kwa mwerezi katika Lebanuni, kusema, 'Mpatie mwanangu binti yako amuoe; lakini hayawani aliyekuwako Lebanoni akaukanyaga chini ule mbaruti.

10Umempiga sana Edomu, na moyo wako umekuinua. Jisifu katika ushindi wako, lakini kaa nyumbani, kwa nini unataka kujisababishia mataizo na kuanguka, wote wewe na Yuda pamoja nawe?”

11Lakini Amazia hakutaka kusikia. Hivyo Yehoashi mfalme wa Israeli akakwea yeye na Amazia mfalme wa Yuda wakakutana uso kwa uso huko Beth Shemeshi, ambayo ilikuwa ya Yuda.

12Yuda walishindwa mbele ya Israeli, na kila mtu akakimbia nyumbani.

13Yehoashi mfalme wa Israeli, akamchukua Amazia, mfalme wa Yuda mwana wa Yehoashi mwana wa Ahazia, huko Beth Shemeshi. Akaja Yerusalemu na kuuangusha chini ukuta wa Yerusalemu kutoka lango la Efraimu mpaka kwenye pembe ya lango, urefu wa mbali wa dhiraa mia nne.

14Akachukua dhahabu na fedha zote, na vitu vyote ambavyo vilipatikana katika nyumba ya Yahwe, na vitu vya thamani kwenye nyumba ya mfalme, pamoja na mateka pia, na kurudi samaria.

15Kama ilivyo kwa mambo mengine yamhusuyo Yehoashi, yote aliyoyafanya, ushujaa wake, na jinsi alivyopigana na Amazia mfalme wa Yuda, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya mfalme wa Israeli?

16Kisha Yehoashi akalala na wazee wake na ailizikwa katika Samaria pamoja na wafalme wa Israeli, na Yeroboamu, mwanaye, akawa mfalme katika eneo lake.

17Amazia mwana wa Yoashi, mfalme wa Yuda, akaishi miaka kumi na tano baada ya Yehoashi mwana wa Yehoahazi, mfalme wa Israeli.

18Kama ilivyo kwa mambo mengine yanayomhusu Amazia, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya mfalme wa Yuda?

19Wakafanya njama dhidi ya Amazia katika Yerusalimu, akakimbilia Lakishi. Akakimbia hadi Lakishi, lakini wakawatuma watu kumfuata hadi Lakishi na kumuua huko.

20Wakamrudisha kwa farasi, na alizikwa pamoja na wazee wake katika mji wa Saudi.

2 Mambo ya Nyakati

2 Nya 25:1–28

1Amaza alikuwa na umri wa amiaka ishirini na na tano alipoanza kutawala; alitawala miaka ishini na tisa katika Yerusalemu. Jina la mama yake lilikuwa Yehoadani, wa Yerusalemu.

2Alifanya yaliyokuwa sahihi katika macho ya Yahwe, lakini siyo kwa moyo uliojitoa kikamilifu.

3Ikawa kwamba mapema utawala wake ulipokuwa umeimarika, aliwaua watumishi ambao walikuwa wamemuua baba yake, mfalme.

4Lakini hakuwaua watoto wa wale wauaji, bali alitenda kama kama ilivyoaandikwa katika sheria, katika kitabu cha Musa, kama Yahwe alivyokuwa ameamru. “Baba hatajuta kwa ajili ya watoto, wala watoto hawatakufa kwa ajili ya baba zao. Badala yake, kila mtu lazima afe kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe”.

5Aidha, Amazia aliwakusanya Yuda pamoja, na akawaandikisha kwa kufuata nyumba za babu zao, chini ya maakida wa maelfu na maakida wa mamia —wote wa Yuda na wa Benyamini. Akawahesabu kuanzia wa mika ishirini na kuendelea, na akawaona wako 300,000 wanaume waliochaguliwa, wawezaoa kwenda vitani, walioweza kushika mkuki na ngao.

6Pia alikodi wanaume wa kupigana 100,000 kutoka Israeli kwa fedha mia moja.

7Lakini mtu wa Mungu alikuja kwake na kusema, “ Mfalme, usiliache jeshi la Istaeli kwenda nawe, kwa maana Yahwe hayupo pamoja na Israeli -wala na mtu Yeyote wa Efraimu.

8Lakini hata kama mtaenda na mkiwa wenye ushupavu na imara katika vita, Mungu atawatupa chini mbele ya adui, kwa maana Mungu ana nguvu za kusaidia, na nguvu za kurusha chini”.

9Amazia akasema kwa mtu wa Mungu, “Lakini tutafanyaje kuhusu talanta mia moja nilizowapa jeshi la Israeli? Mtu wa Mungu akajibu, Yahwe anauwezo wa kukupa vingi zaidi kuliko hivyo.”

10Kwa hiyo Amazia akalitenganisha jeshi lilokuja kwake kutoka Efraimu; akawarudisha nyumbani tena. Hivyo hasira yao iliwaka sana zidi ya Yuda, na walirudi nyumbani kwa hasara kali.

11Amazia akajipa ujasiri na kuwaongoza watu wake kwenda nje kwenye bonde la chumvi, huko akawashinda wanaueme elfu kumi wa Seiri.

12Jeshi la Yuda likawachukua elfu kumi wengine wakiwa hai. Wakawapeleka juu ya mwamba na kuwarushwa chini kutoka huko, hivyo wote wakavunjika vunjika katika vipande.

13Lakini watu wa jeshi ambalo Amazia alilirudisha, ili kwamba wasiende naye vitani, wakauvamia mji Yuda kuanzia Somaria hadi Beth- horoni. Wakawapiga watu elfu tatu na kuwateka wengi sana.

14Sasa ikawa kwamba baada ya Amazia kurudi kutoka kuwachinja Waedomu, akaileta miungu ya watu wa Seiri, na kuisimamisha iwe miungu yake. Akainama chini mbele ya hiyo miungu na kuitolea sadaka za uvumba.

15Hivyo hasira ya Yahwe ikawaka zidi ya Amazia. Akamtuma nabii kwake, ambaye alisema, “Kwa nini umeitafuta miungu ya watu ambayo haikuwaokoa hata watu wake yenyewe zidi ya mkono wako?”

16Akiwa kwamaba yule nabii alipokuwa anaongea naye, mfalme akamwambia, “Je, wewe tumekufanya kuwa mshauri wa mfalme? Acha! Kwa nini ujitakie kuuawa?” Kisha nabii akaacha na kusema, ninajua kwamba Mungu ameamua kukuangaamiza kwa sababu umefanya tendo hili na hujasikilisa ushauri wangu.”

17Kisha Amazia akashauriana na washauri na kutuma wajumbe kwa Yehoashi mwana wa Yehoahazi mwana wa Yehu, mfalme wa Israel. akisema, “Njoni, tukutane uso kwa uso katika vita”.

18Lakini Yehoashi mfalme wa Israeli akatuma wajumbe kwa Amaziahi mfalme wa Yuda, akisema, Mbaruti uliokuwa Lebanoni ulituma ujumbe kwa mwerezi ulioko Lebanoni, ukisema, Mtoe binti yako kwa mwanangu awe mke wake; lakini akapita hayawani katika Lebanoni akatembea na kuukanyaga chini mbaruti.

19Umesema, 'Ona, nimeipiga Edomu,' na moyo wako umekuinua juu. Jipe fahari katika ushindi wako, lakini ukae nyumbani, kwa maana ni kwa nini ujisababishie matatizo mwenyewe na kuanguka, wote wewe na Yuda pamoja nawe?'

20Lakini Amazia hakusikiliza, kwa sababu tukio hili lilikuwa limetoka kwa Mungu, ili awatie Waisraeli katika mkono wa adui zao, kwa sababu walikuwa wametafuta ushauri kutoka kwa miungu ya Edomu.

21Kwa hiyo, Yehoashsi, mfalme wa Israeli, akavamia; yeye na Amazia, mfalme wa Yuda, wakakutana uso kwa uso huko Beth -shemishi, ulioko Yuda.

22Yuda akashindwa mbele za Israeli, na kila mtu akarudi nyumbani.

23Yehoashi, mfalme wa Israeli, akamkamata Amazia mwana wa Yehoashi mana wa Ahazia, mfalme wa Yuda, huko Beth - shemeshi. Akamleta Yerusalemu na kuuangusha chini ukuta wa Yerusalemu kuanzia Lango la Efraimu hadi kona ya Lango, umbali wa mikono mia nne.

24Akachukua dhahabu na fedha zote, vitu vyote vilivyoonekana akatika nyumba aya Mungu kwa Obedi Edomu, na vitu vya thamanai katika nyumba ya mfalme, na mateka pia, na akarudi Samaria.

25Amazia mwana wa Yoashi, mfalme wa Yuda, aliishi miaka kumi na tano baada ya kifo cha Yehoashi, mwana wa Yehoahazi, mfalme wa Israeli.

26Kwa mambo mengingine kuhusu Amzia, mwanzo na mwisho, tazama, je, hayajaandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli?

27Sasa kutoka wakati amabaoa Amazia aligeukia mbali asimfuate Yahwe, walianza kupanga njama zidi yake katika Yerusalemu. Akakimbilia Lachishi, lakini wakatuma watu nyuma yake wamfuate Lachishsi na walimuua huko.

28Wakamleta juu ya farasis na wakamzika pamoja na babu zake kataika Mji wa Yuda.

Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.

Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY