Gundua › Injili kando kwa kando › Mafundisho
Injili kando kwa kando · Mafundisho
Kondoo aliyepotea
Mt 18:12–14 · Lk 15:3–7
Mt 18:12–1412Mnafikiri nini? Ikiwa mtu ana kondoo mia moja, na mmoja wao akapotea, je hatawaacha tisini na tisa ya mlimani na kwenda kumtafuta mmoja aliyepotea?
13Na akiisha kumpata, kweli nawaambieni, anamfurahia kuliko wale tisini na tisa wasiopotea.
14Vivyo hivyo, siyo mapenzi ya Baba yenu wa mbinguni kuwa mmoja wa wadogo hawa aangamie.
Lk 15:3–73Yesu akasema mfano huu kwao, akisema
4“Nani kwenu, kama ana kondoo mia moja na akipotelewa na mmoja wao, hatawaacha wale tisini na tisa nyikani, na aende akamtafute yule aliyepotea hadi amwone?
5Naye akisha kumpata humweka mabegani pake na kufurahia.
6Afikapo kwenye nyumba, huwaita rafiki zake na jirani zake akawaambia furahini pamoja nami, kwa kuwa nimempata kondoo wangu aliyepotea.'
7nawaambia vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, zaidi ya wenye haki tisini na tisa ambao hawana haja ya kutubu
Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.
Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY