Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Desemba 2027 › 21 Desemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 8 Desemba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 21 Desemba 2027
Jumanne · Wiki ya 27 baada ya Pentekoste · Sauti ya 1
Sikukuu na watakatifu
Mtakatifu Mtawa Patapio (karne ya 7)
Mfungo wa Kuzaliwa kwa Bwana
Mfungo: pamoja na mafuta
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
11Lakini kwa wale wajane vijana, kataa kuwaandikisha kwenye orodha ya wajane. Kwa kuwa wakiingia kwenye matamanio ya kimwili dhidi ya Kristo, wanataka kuolewa. 12Kwa njia hii huingia kwenye hatia kwa kuwa huvunja kujitoa kwao kwa awali. 13Na pia huingia kwenye mazoea ya uvivu. Wao huzunguka nyumba kwa nyumba. Si tu kwamba ni wavivu, bali pia huwa wasengenyaji na na wenye kuingilia mambo ya wengine. Wao husema mambo wasiyopaswa kuyasema. 14Kwa hiyo mimi nataka wanawake vijana waolewe, wazae watoto, wasimamie nyumba zao, ili kutokumpa adui nafasi ya kutushitaki kwa kufanya dhambi. 15Kwa sababu baadhi yao wameshamgeukia Shetani. 16Kama mwanamke yeyote aaminiye ana wajane, basi na awasaidie, ili kanisa lisilemewe, ili liweze kuwasaidia wale walio wajane kweli kweli. 17Basi wazee wale watawalao vyema wahesabiwe kuwa wamestahili heshima maradufu, hasa wale wanaojishughulisha na kufundisha neno la Mungu. 18Kwa kuwa maandiko yanasema, “Usimfumbe ng'ombe kinywa apulapo nafaka,” na “Mfanya kazi anastahili mshahara wake.” 19Usipokee mashitaka dhidi ya mzee isipokuwa kuna mashahidi wawili au watatu. 20Waonye wakosaji mbele ya watu wote ili wengine waliobaki labda wataogopa. 21Nakuagiza kwa dhati mbele ya Mungu, na mbele ya Kristo Yesu, na malaika wateule, kwamba uzitunze maagizo haya bila ubaguzi wowote, na kwamba usifanye jambo lolote kwa upendeleo.
Injili
12Lakini kabla ya mambo haya yote, wataweka mikono yao juu yenu na kuwatesa, kuwapeleka kwenye masinagogi na magereza, kuwaleta mbele za wafalme na wenye mamlaka kwa sababu ya jina langu. 13Hii itawafungulia fursa kwa ushuhuda wenu. 14Kwahiyo amueni mioyoni mwenu kutoandaa utetezi wenu mapema, 15kwa sababu nitawapa maneno na hekima, ambayo adui zenu wote hawataweza kuipinga au kuikana. 16Lakini mtakataliwa pia na wazazi wenu, ndugu zenu, jamaa zenu na rafiki zenu, na watawaua baadhi yenu. 17Mtachukiwa na kila mmoja kwa sababu ya jina langu. 18Lakini hakuna hata unywele mmoja wa vichwa vyenu utakaopotea. 19Katika kuvumilia mtaziponya nafsi zenu.
Watakatifu wa siku
- Mfiadini wa Kikasisi Sergio, padri (1937)
- Mitume Sosthene, Apolo, Kefa, Tikiko, Epafrodito, Kaisari na Onesiforo, wa Mitume 70 (karne ya 1)
- Wafiadini 62, mapadri, na walei 300, walioteswa na Waariani huko Afrika (477)
- Mtakatifu Mtawa Kirilo wa Chelmogorsk (1368)
- Mfiadini Anthusa huko Roma (karne ya 5)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 8 Desemba katika kalenda ya kanisa ni 21 Desemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki