Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Desemba 2027 › 16 Desemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 3 Desemba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 16 Desemba 2027
Alhamisi · Wiki ya 26 baada ya Pentekoste · Sauti ya 8
Sikukuu na watakatifu
Nabii Sefania (635-605 K.K.)
Mfungo wa Kuzaliwa kwa Bwana
Mfungo: pamoja na mafuta
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
1Usemi huu ni wakuaminika: Kama mtu anatamani kuwa Msimamizi, anatamani kazi njema. 2Kwa hiyo msimamizi ni lazima asiwe na lawama. Ni lazima awe mume wa mke mmoja. Ni lazima awe na kiasi,, busara, mwenye utaratibu, mkarimu. Ni lazima awe uwezo wa kufundisha. 3Asiwe anatumia mvinyo, asiwe mgomvi, bali mpole, mwenye amani. Ni lazima asiwe mwenye kupenda fedha. 4Inampasa kuwasimamia vema watu wa nyumbani mwake mwenyewe, na watoto wake imewapasa kumtii kwa heshima zote. 5Maana ikiwa mtu hajui kuwasimamia watu wa nyumbani mwake mwenyewe, atalileaje kanisa la Mungu? 6Asiwe mwamini mpya, ili kwamba asije akajivuna na kuanguka katika hukumu kama yule mwovu. 7Lazima pia awe na sifa njema kwa wote walioko nje, ili asije akaanguka kwenye aibu na mtego wa mwovu. 8Mashemasi, vilevile wanapaswa kuwa wenye kustahili heshima, wasiwe wenye kauli mbili. Wasitumie mvinyo kupita kiasi au kuwa na tamaa. 9Waweze kuitunza kwa dhamiri safi ile kweli ya imani iliyofunuliwa. 10Wawe pia wamethibitishwa kwanza, halafu waweze kuhudumu kwa sababu hawana lawama. 11Wanawake vivyo hivyo wawe wenye heshima. Wasiwe wasingiziaji. Wawe na kiasi na waaminifu kwa mambo yote. 12Mashemasi ni lazima wawe waume wa mke mmoja mmoja. Lazima waweze kuwasimamia vema watoto wao na wa nyumbani mwao. 13Kwa kuwa wale wanaotumika vizuri hupata msimamo mzuri na ujasiri mkubwa katika imani iliyo katika Kristo Yesu.
Injili
9Aliwaambia watu mfano huu, “Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu, akalikodisha kwa wakulima wa mizabibu, na akaenda nchi nyingine kwa muda mrefu. 10Kwa muda uliopangwa, alimtuma mtumishi kwa wakulima mizabibu, kwamba wampe sehemu ya matunda ya shamba la mizabibu. Lakini wakulima wa mzabibu wakampiga, wakamrudisha mikono- mitupu. 11Kisha akamtuma tena mtumishi mwingine na nao wakampiga, kumtendea vibaya, na wakamrudisha mikono- mitupu. 12Alimtuma tena wa tatu na nao wakamjeruhi na kumtupa nje. 13Hivyo bwana wa shamba akasema, 'Nitafanya nini? Nitamtuma mwanangu mpendwa. Labda watamheshimu. ' 14Lakini wakulima wa mzabibu walipomwona, walijadili wao kwa wao wakisema, 'Huyu ndiye mrithi. Tumuue, ili urithi wake uwe wetu. ' 15Wakamtoa nje ya shamba la mizabibu na kumuua. Je bwana shamba atawafanya nini? 16Atakuja kuwaangamiza wakulima wa mzabibu, na atawapa shamba hilo wengine”. 'Nao waliposikia hayo, wakasema, 'Mungu amekataa' 17Lakini Yesu akawatazama, akasema, “Je andiko hili lina maana gani? 'Jiwe walilolikataa wajenzi, limekuwa jiwe la pembeni'? 18Kila mtu aangukaye juu ya jiwe hilo, atavunjika vipande vipande. Lakini yule ambaye litamwangukia, litamponda. '
Watakatifu wa siku
- Mtakatifu Mtawa Sava wa Storozhi (wa Zvenigorod) (1406)
- Mfiadini wa Kikasisi Andrea, padri (1920)
- Mfiadini wa Kikasisi Nikolao, padri (1937)
- Mtakatifu Georgi Mwungamaji (1960)
- Mtakatifu Mtawa Theodulo wa Konstantinopoli (karibu 440)
- Mtakatifu Mtawa Yohana, mnyamavu, aliyekuwa Askofu wa Kolonia (558)
- Mfiadini wa Kikasisi Theodoro, Askofu Mkuu wa Aleksandria (606)
- Mtakatifu Mtawa Georgi wa Chernika
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 3 Desemba katika kalenda ya kanisa ni 16 Desemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki