Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Desemba 2027 › 14 Desemba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 14 Desemba 2027
Jumanne · Juma la 3 la Majilio
Sikukuu na watakatifu
Jumanne ya Juma la 3 la Majilio
Kumbukumbu · Rangi ya liturujia: nyeupe
Mt. Yohane wa Msalaba, padre na mwalimu wa Kanisa · Kumbukumbu
Masomo ya siku
Somo la kwanza
1Ole kwa mji ulioasi! Mji wenye vurugu umenajisiwa. 2Haukuisikiliza sauti ya Mungu, wala haukupokea masahihisho kutoka kwa Yahwe. Hakumtumaini Yahwe na hatamkaribia Mungu wake. 9Ndipo nitawapa midomo safi watu, kuwaita wote kwa jina la Bwana kunitumikia wakisimama bega kwa bega. 10Kutoka ng'ambo ya mto Ethiopia waniabuduo - watu wangu waliotawanyika - wataleta dhabihu kwa sababu yangu. 11Katika siku hiyo hamtawekwa kwenye woga kwa matendo yenu yote ambayo mmeyafanya dhidi yangu, tangu wakati ule nitaondoa kutoka kwenu wale waliosherehekea fahari yenu, na kwa sababu hamtakuwa na muda mrefu kufanya majivuno juu ya mlima wangu mtakatifu. 12Lakini nitawaacha kama wa chini zaidi na watu masikini, na mtapata kimbilio katika jina la Yahwe. 13Mkazi wa Israeli si muda mrefu hatafanya udhalimu au kusema uongo, na hakuna ulimi wa udanganyifu utakaoonekana mdomoni mwao; hivyo watalisha na kulala chini, na hakuna hata mmoja atakayewafanya kuogopa.”
Wimbo wa katikati
1Zaburi ya Daudi; wakati alipojifanya kuwa mwendawazimu mbele ya Abimeleki, ambaye alimtoa yeye nje. Nitamsifu Yahwe wakati wote, siku zote sifa zake zitakuwa mdomoni mwangu. 2Nitamsifu Yahwe! walio onewa wasikie na kufurahi. 5Wale wanao mtazama yeye wana furaha, na nyuso zao hazina aibu. 6Huyu mtu aliye onewa alilia na Yahwe akamsikia na kumuokoa kwenye matatizo yake yote. 16Uso wa Yahwe uko kinyume na wale watendao uovu, kuikatilia mbali kumbukumbu yao duniani. 17Wenye haki hulia na Yahwe husikia na kuwaokoa kwenye matatizo yao yote. 18Yahwe yu karibu nao waliovunjika moyo, naye huwaokoa waliogandamizwa rohoni. 22Yahwe huokoa maisha ya watumishi wake. Hakuna atakaye hukumiwa hata mmoja atafutaye usalama katika yeye.
Injili
28Lakini mnafikiri nini? Mtu mwenye wana wawili. Akaenda kwa moja na kumwambia, 'Mwanangu, nenda ukafanye kazi katika shamba la mizabibu 29leo. 'Mwana akajibu na kusema, 'sitakwenda, ' Lakini baadaye akabadilisha mawazo yake na akaenda. 30Na Mtu yule akaenda kwa mwana wa pili na kusema kitu kilekile. Mwana huyu akajibu na kusema, 'nitakwenda, bwana', lakini hakwenda. 31Yupi kati ya wana wawili aliyefanya matakwa ya baba yake? Wakasema, “Mwana wa kwanza.” Yesu akawaambia, “Kweli nawaambieni, wakusanya ushuru na makahaba wataingia kwenye ufalme wa Mungu kabla yenu kuingia. 32Kwa maana Yohana alikuja kwenu kwa njia iliyo nyoofu, lakini hamkumwamini, wakati wakusanya ushuru na makahaba walimwamini. Na ninyi, mlipoona hilo likitendeka, hamkuweza kutubu ili baadaye mumwamini.
Watakatifu wa siku
- Mt. Yohane wa Msalaba, padre na mwalimu wa Kanisa
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili C, mwaka wa siku za kazi II.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki