Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Desemba 2027 › 2 Desemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 19 Novemba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 2 Desemba 2027
Alhamisi · Wiki ya 24 baada ya Pentekoste · Sauti ya 6
Sikukuu na watakatifu
Nabii Obadia (mmoja wa manabii 12) (karne ya 9 K.K.)
Mfungo wa Kuzaliwa kwa Bwana
Mfungo: pamoja na mafuta
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
1Sasa, kwa habari ya muda na nyakati, ndugu, hamna haja kwamba kitu chochote kiandikwe kwenu. 2Kwa kuwa ninyi wenyewe mwajua kwa usahihi ya kuwa siku ya Bwana inakuja kama mwizi ajapo usiku. 3Pale wasemapo kuna “Amani na usalama”, ndipo uharibifu huwajia ghafla. Ni kama utungu umjiavyo mama mwenye mimba. Hawataepuka kwa njia yeyote. 4Lakini ninyi, ndugu hampo kwenye giza hata ile siku iwajie kama mwizi. 5Kwa maana ninyi nyote ni wana wa nuru na wana wa mchana. Sisi siyo wana wa usiku au wa gizani. 6Hivyo basi, tusilale kama wengine walalavyo. Bali tukeshe na kuwa makini. 7Kwa kuwa wanaolala hulala usiku na wanao lewa hulewa usiku. 8Kwa kuwa sisi ni wana wa mchana, tuwe makini. Tuvae ngao ya imani na upendo, na, kofia ya chuma, ambayo ni uhakika wa wokovu wa wakati ujao.
Injili
1Yesu aliwaambia tena wanafunzi wake, “Palikuwa na mtu mmoja tajiri aliyekuwa na meneja, na alitaarifiwa ya kwamba meneja huyu anatapanya mali zake. 2Hivyo tajiri akamwita, akamwambia, “Ni nini hii ninayo isikia juu yako? Toa hesabu ya umeneja wako, kwa kuwa huwezi kuwa meneja tena.' 3Yule meneja akasema moyoni mwake, Nifanye nini, maana bwana wangu ananiondolea kazi yangu ya umeneja? Sina nguvu za kulima, na kuomba naona haya. 4Najua nitakalotenda ili nitakapotolewa katika kazi yangu ya uwakili watu wanikaribishe nyumbani mwao. 5Hivyo wakili akawaita wadeni wa bwana wake kila mmoja akamwambia wa kwanza, 'unadaiwa kiasi gani na bwana wangu?' 6Akasema vipimo mia moja vya mafuta akamwambia 'chukua hati yako keti upesi andika hamsini.' 7kisha akamwambia mwingine na wewe unadaiwa kiasi gani?' akasema 'vipimo mia moja vya unga vya ngano.' Akamwambia 'twaa hati yako andika themanini.' 8Yule bwana akamsifu meneja dhalimu kwa vile alivyotenda kwa wereu. Kwakua watoto wa ulimwengu huu ni werevu nyingi na hushughulika kwa ujanja na watu wa upande wao kuliko walivyo watoto wa nuru. 9Nami nawaambia jifanyieni marafiki kwa mali ya udhalimu ili itakapokosekana wawakaribishe katika makao ya milele.
Watakatifu wa siku
- Mfiadini Barlaamu (karibu 304)
- Watakatifu Watawa Barlaamu na Yoasafu, mwana wa mfalme wa India, na baba yake Mfalme Abeneri (karne ya 4)
- Askofu Mtakatifu Filareti, Mitropoliti wa Moscow (1867)
- Wafiadini wa Kikasisi Porfirio, Askofu wa Simferopol, Sergio, Mikaeli, Aleksanda, Yohana, Konstantino, Aleksanda, Ignatio, Simeoni, Yohana, Yohana, Demetrio, Yakobo, Yakobo, mapadri, Watawa Wafiadini Yoasafu, Genadi, Petro, Gregori, Benyamini, Gerasimo, Mikaeli, Wafiadini Valentino, Petro, Leonida, Timotheo (1937)
- Mfiadini Iliodoro (karibu 273)
- Mfiadini Aza na pamoja naye askari 150 (284-305)
- Mtakatifu Mtawa Hilarioni wa Georgia, mtenda miujiza (875)
- Mtakatifu Mtawa Barlaamu, abati wa Mapango ya Kyiv (1065)
- Kupatikana kwa masalia ya Mtawa Mfiadini Adriani wa Poshekhonye, wa Yaroslavl (1625)
- Ikoni ya Mama wa Mungu iitwayo “Faraja katika Huzuni na Masikitiko” (1863)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 19 Novemba katika kalenda ya kanisa ni 2 Desemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki