Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2027 › 24 Novemba

Kalenda ya Kiorthodoksi · 11 Novemba (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 24 Novemba 2027

Jumatano · Wiki ya 23 baada ya Pentekoste · Sauti ya 5

Sikukuu na watakatifu

Mfiadini Mkuu Mina (304)

Siku ya mfungo

Mfungo: pamoja na mafuta

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Waraka

1 The 2:1–8

1Kwa kuwa ninyi wenyewe mnajua, ndugu, kuwa ujio wetu kwenu haukuwa wa bure. 2Mnajua kwamba mwanzoni tuliteseka na walitutenda kwa aibu kule Filipi, kama mujuavyo. Tulikuwa na ujasiri katika Mungu kunena injili ya Mungu hata katika taabu nyingi. 3Kwa maana mahusia yetu hayatokani na ubaya, wala katika uchafu, wala katika hila. 4Badala yake, kama vile tulivyokubalika na Mungu na kuaminiwa injili, ndivyo tunenavyo. Tunanena, si kwa kuwafurahisha watu, lakini kumfurahisha Mungu. Yeye pekee ndiye achunguzaye mioyo yetu. 5Kwa maana hatukutumia maneno ya kujipendekeza wakati wote wote, kama mjuavyo, wala ukutumia maneno kama kisingizio kwa tamaa, Mungu ni shahidi wetu. 6Wala hatukutafuta utukufu kwa watu, wala kutoka kwenu au kwa wengine. Tungeweza kudai kupendelewa kama mitume wa Kristo. 7Badala yake tulikuwa wapole kati yenu kama mama awafarijivyo watoto wake mwenyewe. 8Kwa njia hii tulikuwa na upendo kwenu. Tulikuwa radhi kuwashirikisha si tu injili ya Mungu bali pia na maisha yetu wenyewe. Kwa kuwa mmekuwa wapendwa wetu.

Injili

Lk 12:48–59

48Lakini mtumishi asiyejua mapenzi ya bwana wake, lakini akafanya yanayostahili adhabu, atapigwa viboko vichache. Kwa kuwa yeye aliyepewa vingi, vingi hudaiwa kutoka kwake, na yeye aliyeaminiwa kwa vingi, kwake vitadaiwa vingi zaidi. 49Nimekuja kuwasha moto duniani, na natamani iwe umekwishawaka, 50Lakini nina ubatizo ambao nitabatizwa, na nina huzuni mpaka utkapokamilika! 51Je mnafikiri kuwa nimekuja kuleta amani duniani? Hapana, Nawaambieni, badala yake nimeleta mgawanyiko. 52Tangu sasa na kuendelea kutakuwa na watu watano katika nyumba moja wamegawanyika, na watatu watakuwa kinyume na wawili, na wawili watakuwa kinyume na watatu. 53Watagawanyika, baba atakuwa kinyume na mwanae, na mwanae atakuwa kinyume na babaye, mama atakuwa kinyume na binti yake, na binti atakuwa kinyume na mama yake, Mama mkwe atakuwa kinyume na mkwe wake naye mkwe atakuwa kinyume na mama mkwe wake. 54Yesu akawa anawaambia makutano pia, “Mara muonapo mawingu yakitokea magharibi, mnasema nyakati za mvua zimewadia; na ndivyo inavyo kuwa, 55Na upepo wa kusini ukivuma, mnasema, Patakuwepo na joto kali, na ndivyo inavyokuwa. 56Enyi wanafiki, mnaweza kutafsiri mwonekano wa nchi na anga, lakini inakuwaje hamuwezi kuutafsiri wakati uliopo? 57Ni kwa nini kila mmoja wenu asipambanue lililo sahihi kwake kulifanya wakati ambapo angali na nafasi ya kufanya hivyo? 58Maana mkienda na mshitaki wako mbele ya hakimu, jitahidi kupatana na mshitaki wako mungali bado mko njiani asije akakupeleka kwa hakimu, na hakimu akupeleka kwa ofisa, na ofisa akakutupa gerezani. 59Nakuambia, hutatoka huko hadi umelipa mpaka senti ya mwisho.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 24 Novemba

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 11 Novemba katika kalenda ya kanisa ni 24 Novemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki