Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2027 › 3 Novemba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 3 Novemba 2027

Jumatano · Juma la 31 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumatano ya Juma la 31 la Mwaka

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani

Mt. Martino wa Porres, mtawa · Kumbukumbu ya hiari

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Rum 13:8–10

8Msidaiwe na mtu kitu chochote, isipokuwa kupendana ninyi kwa ninyi. Kwa kuwa yeye ampendaye jirani yake ametimiliza sheria. 9Kwa kuwa, “Hautazini, hautaua, hautaiba, hautatamani,” na kama kuna amri nyingine pia, imejumlishwa katika sentensi hii: “Utampenda jirani yako kama wewe mwenyewe.” 10Upendo hamdhuru jirani wa mtu. Kwa hiyo, upendo ni ukamilifu wa sheria.

Wimbo wa katikati

Zab 112:1–2, 4–5, 9

1Msifuni Yahwe. Amebarikiwa mtu yule anaye mtii Yahwe, apendezwaye sana na amri zake. 2Kizazi chake kitakuwa ni chenye nguvu duniani; kizazi cha mcha Mungu kitabarikiwa. 4Nuru huangazia gizani kwa ajili ya mtu mcha Mungu; yeye ni wa fadhili, huruma, na haki. 5Heri atendaye fadhili na kukopesha, afanyaye mambo yake kwa uaminifu. 9Huwapa masikini kwa ukarimu; haki yake yadumu milele; atainuliwa kwa heshima.

Injili

Lk 14:25–33

25Sasa umati mkubwa walikuwa wanakwenda pamoja naye, naye akageuka na akawaambia, 26'Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, mama yake, mke wake, watoto wake, ndugu zake waume na wanawake- ndio, na hata maisha yake pia -hawezi kuwa mwanafunzi wangu. 27Mtu asipochukua msalaba wake na kuja nyuma yangu hawezi kuwa mwanafunzi wangu. 28Maana ni nani kati yenu, ambaye anatamani kujenga mnara hataketi kwanza akadirie gharama kwa mahesabu kama ana kile anachohitaji ili kukamilisha hilo? 29Vinginevyo, baada ya kuweka msingi na kushindwa kumaliza, wote walioona wataanza kumdhihaki, 30wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza.' 31Au mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine katika vita, ambae hatakaa chini kwanza na kuchukua ushauri kuhusu kama ataweza, pamoja na watu elfu kumi kupigana na mfalme mwingine anayekuja juu yake na watu elfu ishirini? 32Na kama sivyo, wakati jeshi la wengine bado liko mbali, hutuma balozi kutaka masharti ya amani. 33Kwa hiyo basi, yeyote kati yenu ambaye hataacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 3 Novemba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki