Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2027 › 1 Novemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 19 Oktoba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 1 Novemba 2027
Jumatatu · Wiki ya 20 baada ya Pentekoste · Sauti ya 2
Sikukuu na watakatifu
Mwenye Haki Yohana wa Kronstadt, mtenda miujiza (ROCOR) (1908)
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
12Kwa hiyo basi, wapendwa wangu kama mnavyotii siku zote, Si tu katika uwepo wangu lakini sasa ni zaidi sana hata pasipo uwepo wangu, uwajibikeni wokovu wenu wenyewe kwa hofu na kutetemeka. 13Kwa kuwa ni Mungu anayetenda kazi ndani yenu ili kuwawezesha kunia na kutenda mambo yale yampendezayo yeye. 14Fanyeni mambo yote bila malalamiko na mabishano. 15Fanyeni hivyo ili kwamba msilaumike na kuwa watoto wa Mungu waaminifu wasiyo na lawama. Fanyeni hivyo ili kwamba muwe nuru ya dunia, katika kizazi cha uasi na uovu. 16Shikani sana neno la uzima ili kwamba niwe na sababu ya kutukuza siku ya Kristo. Kisha nitafahamu kwamba sikupiga mbio bure wala sikutaabika bure.
Injili
18Nayo ikawa kwamba, alipokuwa akiomba peke yake, wanafunzi wake walikuwa pamoja naye, na akawauliza akisema, “watu husema mimi ni nani?” 19Wakijibu, wakasema, “Yohana mbatizaji, lakini wengine husema Eliya, na wengine husema mmoja wa manabii wa nyakati za zamani amefufuka tena.” 20Akawambia, “Lakini ninyi mwasema mimi ni nani?” Akijibu Petro akasema, “Kristo kutoka kwa Mungu.” 21Lakini kwa kuwaonya, Yesu akawaelekeza kutomwambia yeyote juu ya hili, 22akasema kwamba mwana wa Adamu lazma ateseke kwa mambo mengi na kukataliwa na wazee na Makuhani wakuu na waandishi, na atauawa, na siku ya tatu atafufuka.
Watakatifu wa siku
- Nabii Yoeli (800 K.K.)
- Mfiadini Uaro na pamoja naye wafiadini saba, walimu wa Kikristo (karibu 307)
- Kuhamishwa kwa masalia ya Mtakatifu Mtawa Yohana wa Rila (1238)
- Mfiadini wa Kikasisi Sergio, padri (1937)
- Mbarikiwa Kleopatra (327) na mwanawe Yohana (320)
- Mfiadini wa Kikasisi Sadoki (Shah-Dust), Askofu wa Uajemi, na pamoja naye wafiadini 128 (342-344)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 19 Oktoba katika kalenda ya kanisa ni 1 Novemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki