Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2027 › 1 Novemba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 1 Novemba 2027

Jumatatu · Juma la 31 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Watakatifu Wote

Sherehe · Rangi ya liturujia: nyeupe

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Ufu 7:2–4, 9–14

2Nikaona malaika mwingine akija kutoka mashariki, aliyekuwa na muhuri wa Mungu aliye hai. Akalia kwa sauti kuu kwa malaika wanne ambao walipewa ruhusa ya kudhuru nchi na bahari: 3“Msiidhuru nchi, bahari, au miti mpaka tutakapokuwa tumekwishaweka muhuri katika paji za vichwa vya watumishi wa Mungu wetu.” 4Nikasikia idadi ya wale waliotiwa muhuri: 144,000, ambao walitiwa muhuri kutoka kila kabila ya watu wa Israel: 9Baada ya mambo haya nilitazama, na kulikuwa na umati mkubwa ambao hapana mtu angeweza kuuhesabu - kutoka kila taifa, kabila, jamaa, na lugha - wamesimama mbele ya kiti cha enzi na mbele ya Mwanakondoo. Walikuwa wamevaa kanzu nyeupe na wana matawi ya mitende mikononi mwao, 10na walikuwa wakiita kwa sauti ya juu: “Wokovu ni kwa Mungu ambaye ameketi katika kiti cha enzi, na kwa Mwanakondoo!” 11Malaika wote waliokuwa wamesimama kuzunguka kiti cha enzi na kuwazunguka wale wazee pamoja na wenye uhai wanne, wakainama chini ardhini na wakaweka nyuso zao juu ya ardhi mbele ya kiti cha enzi na wakamwabudu Mungu, 12wakisema, “Amina! Sifa, utukufu, hekima, shukurani, heshima, uwezo na nguvu viwe kwa Mungu wetu milele na milele! Amina!” 13Kisha mmoja wa wale wazee akaniuliza, “hawa ni akina nani waliovaa kanzu nyeupe, na wametoka wapi? 14Nikamwambia, “Bwana mkubwa, unajua wewe,” na akaniambia, “Hawa ni wale waliotoka katika dhiki kuu. Wamezifua kanzu zao na kuzifanya nyeupe kwa damu ya Mwanakondoo.

Wimbo wa katikati

Zab 24:1–6

1Zaburi ya Daudi. Nchi ni ya Yahwe, na vyote viijazavyo, dunia, na wote wakaao ndani yake. 2Kwa kuwa yeye aliianzisha juu ya bahari na kuiimarisha juu ya mito. 3Ni nani atakaye panda mlima wa Yahwe? Ni nani atakaye simama patakatifu pake? 4Yeye ambaye ana mikono misafi na moyo safi; ambaye hajauinua uongo, na haja apa kiapo ili kudanganya. 5Yeye atapokea baraka kutoka kwa Yahwe na haki kutoka kwa Mungu wa wokovu wake. 6Kizazi cha wale wamtafutao Mungu ni kama hiki, wale ambao wanautafuta uso wa Mungu wa Yakobo.

Somo la pili

1 Yoh 3:1–3

1Oneni ni pendo la namna gani ametupatia Baba, kwamba tunaitwa watoto wa Mungu, na hivi ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui kwa kuwa haukumtambua yeye. 2Wapendwa sisi sasa ni watoto wa Mungu, na haijadhihirika bado jinsi tutakavyokuwa. Twajua kwamba Kristo atakapoonekana, tutafanana naye, kwani tutamuona kama alivyo. 3Na kila mmoja ambaye ana ujasiri huu kuhusu wakati ujao ulioelekezwa kwake, hujitakasa mwenyewe kama yeye alivyo mtakatifu.

Injili

Mt 5:1–12

1Yesu alipo uona umati, akaondoka na kuelekea Mlimani. Alipokuwa ameketi chini, wanafunzi wake wakaja kwake. 2Akafunua kinywa chake na akawafundisha, akisema, 3“Heri walio maskini wa roho maana ufalme wa mbinguni ni wao. 4Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa. 5Heri wenye upole, maana watairithi nchi. 6Heri wenye njaa na kiu ya haki, maana hao watashibishwa. 7Heri wenye rehema maana hao watapata Rehema. 8Heri wenye moyo safi maana watamwona Mungu. 9Heri wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu. 10Heri wale wanaoteswa kwa ajili ya haki, maana ufalme wa mbinguni ni wao. 11Heri ninyi ambao watu watawatukana na kuwatesa, au kusema kila aina ya ubaya dhidi yenu kwa uongo kwa ajili yangu. 12Furahini na kushangilia, maana thawabu yenu ni kubwa juu mbinguni. Kwa kuwa hivi ndivyo watu walivyo watesa manabii walioishi kabla yenu.

Watakatifu wa 1 Novemba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki