Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2027 › 30 Oktoba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 17 Oktoba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 30 Oktoba 2027
Jumamosi · Wiki ya 19 baada ya Pentekoste · Sauti ya 1
Sikukuu na watakatifu
Nabii Hosea (820 K.K.)
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
58Kwa hiyo, wapendwa kaka na dada zangu, iweni imara na msitikisike. Daima itendeni kazi ya Bwana, kwa sababu mnajua kuwa kazi yenu katika Bwana siyo bure. 16:1Sasa kuhusu michango kwa ajili ya waumini, kama nilivyo elekeza makanisa ya Galatia, vivyo hivyo mwapaswa kufanya. 2Katika siku ya kwanza ya wiki, kila mmoja wenu aweke kitu fulani kando na kukihifadhi, kama muwezavyo. Fanyeni hivyo ili kwamba kusiwe na michango wakati nikija. 3Na nitakapofika, yeyote mtakayemchagua, nitamtuma pamoja na barua kutoa sadaka yenu huko Yerusalem.
Injili
1Sasa ilitokea kwenye Sabato kwamba Yesu alikuwa akipita katika ya shamba la nafaka na wanafunzi wake walikuwa wakichuma masuke, wakayasuguasugua kati ya mikono yao wakala nafaka. 2Lakini baadhi ya Mafarisayo wakasema, “Kwa nini mnafanya kitu ambacho si halali kisheria kukifanya siku ya sabato”? 3Yesu, akawajibu, akisema, “Hamkuwahi kusoma kile Daudi alifanya alipokuwa na njaa, yeye na wanaume waliokuwa pamoja naye? 4Alikwenda katika nyumba ya Mungu, na akachukuwa mikate mitakatifu na kuila baadhi, na kuitoa baadhi kwa watu aliokuwa nao kuila, hatakama ilikuwa halali kwa makuhani kuila.” 5Kisha akawaambia, “Mwana wa Adamu ni Bwana wa Sabato.” 6Ilitokea katika Sabato nyingine kwamba alikwenda ndani ya sinagogi na kuwafundisha watu huko. Palikuwa na mtu ambaye mkono wake wa kulia ulikuwa umepooza. 7Waandishi na Mafarisayo walikuwa wanamwangalia kwa makini kuona kama angemponya mtu siku ya Sabato, ili waweze kupata sababu ya kumshtaki kwa kufanya kosa. 8Lakini alijua nini walikuwa wanafikiri na akasema kwa mtu aliyekuwa amepooza mkono, “Amka, simama hapa katikati ya kila mmoja.” Hivyo huyo mtu akanyanyuka na kusimama pale. 9Yesu akasema kwao, “Nawauliza ninyi, ni halali siku ya Sabato kufanya mema au kufanya madhara, kuokoa maisha au kuyaharibu?” Kisha aliwaangalia wote na kumwambia yule mtu, 10“Nyoosha mkono wako.” Akafanya hivyo, na mkono wake ulikuwa umeponywa.
Watakatifu wa siku
- Mtawa Mfiadini Andrea wa Krete (767)
- Mfiadini wa Kikasisi Neofito, padri, Watawa Wafiadini Hiasintho na Kalisto (1918)
- Mfiadini wa Kikasisi Aleksanda, Askofu Mkuu wa Semipalatinsk (1937)
- Wafiadini Kosma na Damiani wa Uarabuni, matabibu wasiopokea malipo, na ndugu zao Wafiadini Leontio, Anthimo na Eutropio (287 au 303)
- Kuhamishwa kwa masalia ya Mwenye Haki Lazaro wa Siku Nne, Askofu wa Kitioni (898)
- Mtakatifu Mtawa Antoni wa Leokhnovo, wa Novgorod (1611)
- Ikoni za Mama wa Mungu ziitwazo “Bikira Kabla ya Kuzaa na Baada ya Kuzaa” (1827) na “Mkombozi” (karibu 1889)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 17 Oktoba katika kalenda ya kanisa ni 30 Oktoba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki