Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2027 › 5 Oktoba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 22 Septemba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 5 Oktoba 2027
Jumanne · Wiki ya 16 baada ya Pentekoste · Sauti ya 6
Sikukuu na watakatifu
Nabii Yona (karne ya 8 K.K.)
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
11Ndugu, kama naendelea kutangaza tohara, kwanini bado ninateswa? Kwa suala hilo kile ambacho ni kizuizi cha msalaba kitaweza kuharibiwa. 12Ni matakwa yangu kuwa wale wanaowaongoza vibaya watajihasi wenyewe. 13Mungu amewaiteni ninyi, ndugu, kwenye uhuru. Ila msiutumie uhuru wenu kama fursa kwa mwili. Badala yake kwa upendo mhudumiane ninyi kwa ninyi. 14Kwa kuwa sheria yote imekamilika katika amri moja; nayo ni “Ni lazima umpende jirani yako kama wewe mwenyewe.” 15Lakini kama mkiumana na kulana, jiangalieni kwamba msijiharibu ninyi kwa ninyi. 16Nasema, tembeeni kwa roho, na wala hamtazitimiza tamaa za mwili. 17Kwa kuwa mwili una tamaa kubwa dhidi ya Roho, na Roho ina tamaa kubwa dhidi ya mwili. Hizi zinapingana kila moja na nyingine. Matokeo ni kwamba hamfanyi vitu mnavyotamani kuvifanya. 18Lakini kama Roho anawaongoza ninyi, hamko chini ya sheria. 19Sasa matendo ya mwili yanaonekana. Nayo ni uasherati, uchafu, ufisadi, 20ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, husuda, kuwaka hasira, ushindani, faraka, mgawanyiko wa madhehebu, 21wivu, ulevi, ulafi na mambo mengine kama haya. Nawaonya ninyi, kama nilivyowaonya mwanzoni, kwamba wale wanaofanya mambo kama hayo hawataurithi ufalme wa Mungu.
Injili
23Sasa Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, alikuwa na umri upatao miaka thelathini. Alikuwa ni mwana (kama ilivyotadhaniwa) wa Yusufu, mwana wa Eli, 24mwana wa Mathati, mwana wa Lawi, mwana wa Melki, mwana wa Yana, mwana wa Yusufu, 25mwana wa Matathia, mwana wa Amosi, mwana wa Nahumu, mwana wa Esli, mwana wa Nagai, 26mwana wa Maati, mwana wa Matathia, mwana wa Semeini, mwana wa Yusufu, mwana wa Yuda, 27mwana wa Yoanani, mwana wa Resa, mwana wa Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, mwana wa Neri, 28mwana wa Melki, mwana wa Adi, mwana wa Kosamu, mwana wa Elmadamu, mwana wa Eri, 29mwana wa Yoshua, mwana wa Eliezeri,, mwana wa Yorimu, mwana wa Matathi, mwana wa Lawi, 30mwana wa Simeoni, mwana wa Yuda, mwana wa Yusufu, mwana wa Yonamu, mwana wa Eliyakimu, 31mwana wa Melea, mwana wa Mena, mwana wa Matatha, mwana wa Nathani, mwana wa Daudi, 32mwana wa Yese, mwana wa Obedi, mwana wa Boazi, mwana wa Salmoni, mwana wa Nashoni, 33mwana wa Abinadabu, mwana wa Aramu, mwana wa Hesroni,, mwana wa Peresi, mwana wa Yuda, 34mwana wa Yakobo, mwana wa Isaka, mwana wa Ibrahimu, mwana wa Tera, mwana wa Nahori, 35mwana wa Seruig, mwana wa Ragau, mwana wa Pelegi, mwana wa Eberi, mwana wa Sala, 36mwana wa Kenani, mwana wa Arfaksadi, mwana wa Shemu, mwana wa Nuhu, mwana wa Lameki, 37mwana wa Methusela, mwana wa Henoko, mwana wa Yaredi, mwana Mahalalei, mwana wa Kenani, 38mwana wa Enoshi, mwana wa Sethi, mwana wa Adamu, mwana wa Mungu. 4:1Kisha, Yesu akiwa amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Mto Jordani, na aliongozwa na Roho jangwani
Watakatifu wa siku
- Mfiadini wa Kikasisi Foka, Askofu wa Sinopi (117)
- Mtakatifu Mtawa Yona, padri, baba (karne ya 9) wa Watakatifu Theofani, mtunzi wa kanoni, na Theodoro, Walioandikwa Usoni
- Mbarikiwa Paraskeva wa Diveyevo (1915)
- Mfiadini wa Kikasisi Benyamini, Askofu wa Romanov (1930)
- Mfiadini Foka, mtunza bustani (karibu 320)
- Mwenye Haki Petro, aliyekuwa mtoza ushuru (karne ya 6)
- Mtakatifu Mtawa Yona wa Yashezero (1589-1592)
- Mtakatifu Mtawa Makario wa Zhabyn, mtenda miujiza wa Belyov (1623)
- Mfiadini wa Kikasisi Theodosio wa Brazi (1694)
- Mkutano wa Watakatifu wa Tula
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 22 Septemba katika kalenda ya kanisa ni 5 Oktoba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki