Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Septemba 2027 › 21 Septemba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 21 Septemba 2027

Jumanne · Juma la 25 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Mt. Mathayo, mtume na mwinjili

Sikukuu · Rangi ya liturujia: nyekundu

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Efe 4:1–7, 11–13

1Kwa hiyo, kama mfungwa kwa ajili ya Bwana, nawasihi mtembee sawasawa na wito ambao Mungu aliwaita. 2Muishi kwa unyenyekevu mkuu na upole na uvumilivu. Mkichukuliana katika upendo. 3Fanyeni bidii kuutunza umoja wa Roho katika kifungo cha amani. 4Kuna mwili mmoja na Roho moja, kama ambavyo pia mlikuwa mmeitwa katika uhakika wa taraja moja la wito wenu. 5Na kuna Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja, 6na Mungu mmoja na Baba wa wote. Yeye yuko juu ya yote, na katika yote na ndani ya yote. 7Kwa kila mmoja wetu amepewa kipawa kulingana na kipimo cha kipawa cha Kristo. 11Kristo alitoa vipawa kama hivi: mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji, na waalimu. 12Alifanya hivi kuwawezesha waumini kwa ajili ya kazi ya huduma, kwa ajili ya kuujenga mwili wa Kristo. 13Anafanya hivi hadi sisi sote tufikie umoja wa imani na maarifa ya mwana wa Mungu. Anafanya hivi hadi tuweze kukomaa kama wale waliofikia kimo kamili cha Kristo.

Wimbo wa katikati

Zab 19:1–4

1Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi. Mbingu za tangaza utukufu wa Mungu, na mawingu hufanya kazi ya mikono yake ijulikane! 2Siku hadi siku hotuba hutokea; usiku hadi usiku hufunua maarifa. 3Hakuna hotuba wala misemo; sauti zao hazisikiki. 4Bali maneno yao husambaa nje duniani kote, na hotuba zao hata mwisho wa dunia. Yeye ametengeneza hema kwa ajili ya jua kati yao.

Injili

Mt 9:9–13

9Na Yesu alipokuwa akipita kutoka hapo, alimwona mtu ambaye aliitwa kwa jina la Mathayo, ambaye alikuwa amekaa sehemu ya watoza ushuru. Naye akamwambia, “Nifuate mimi” Naye akasimama na kumfuata. 10Na Yesu alipoketi ili ale chakula ndani ya nyumba, wakaja watoza ushuru wengi na watu waovu wakashiriki chakula pamoja na Yesu na wanafunzi wake. 11Ndipo Mafarisayo walipoona hayo, wakawaambia wanafunzi “Kwa nini mwalimu wenu anakula chakula pamoja na watoza ushuru na watu waovu?” 12Yesu aliposikia hayo, naye alisema “ Watu walio na afya nzuri hawahitaji mganga, isipokuwa wale walio wagonjwa. 13Inawapasa muende mkajifunze maana yake, “Ninapenda rehema na siyo dhabihu” Kwa kuwa nilikuja, si kwa wenye haki kutubu, lakini kwa wenye dhambi.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 21 Septemba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki