Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Septemba 2027 › 13 Septemba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 13 Septemba 2027
Jumatatu · Juma la 24 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Jumatatu ya Juma la 24 la Mwaka
Kumbukumbu · Rangi ya liturujia: nyeupe
Mt. Yohane Krisostomo, askofu na mwalimu wa Kanisa · Kumbukumbu
Masomo ya siku
Somo la kwanza
1Kwa hiyo awali ya yote, nahitaji maombi, na dua, na maombezi, na shukrani vifanyike kwa ajili ya watu wote, 2kwa ajili ya wafalme na wote ambao wako kwenye mamlaka, ili kwamba tuweze kuishi maisha ya amani na utulivu katika utauwa wote na heshima. 3Hili ni jema na lenye kukubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu. 4Yeye hutamani kuwa watu wote waokolewe na wapate kuijua kweli. 5Kwa kuwa kuna Mungu mmoja, na kuna mpatanishi mmoja kati ya Mungu na mwanadamu ambaye ni Kristo Yesu. 6Alijitoa mwenyewe kama fidia kwa wote, kama ushuhuda kwa wakati muafaka. 7Kwa sababu hii, mimi mwenyewe nilifanywa kuwa mjumbe wa injili na mtume. Nasema kweli. Sisemi uongo. Mimi ni mwalimu watu Mataifa katika imani na kweli. 8Kwa hiyo, nataka wanaume kila mahali waombe na kuinua mikono mitakatifu bila ghadhabu na mashaka.
Wimbo wa katikati
2Sikia kilio cha kusihi kwangu pale niitapo msaada kutoka kwako, niinuapo mikono yangu mbele ya mahali patakatifu zaidi! 7Yahwe ni nguvu yangu na ngao yangu; moyo wangu wa humwamini yeye, na ninasaidiwa. Kwa hiyo moyo wangu hufurahia sana, nami nitamsifu yeye kwa kuimba. 8Yahwe ni nguvu ya watu wake, naye ni mkombozi salama wa wapakwa mafuta wake. 9Uwaokoe watu wako na uwabariki warithi wako. Uwe mchungaji wao na uwabebe milele.
Injili
1Baada ya Yesu kumaliza kila kitu alichokuwa anasema kwa watu waliomsikiliza, akaingia Kapernaumu. 2Mtumwa fulani wa akida, aliyekuwa wa thamani sana kwake, alikuwa mgonjwa sana na alikuwa karibu ya kufa. 3Lakini akiwa amesikia kuhusu Yesu, yule Akida alimtuma kiongozi wa kiyahudi, kumwomba aje kumwokoa mtumwa wake ili asife. 4Walipofika karibu na Yesu, walimsihi kwa bidii na kusema, “anastahili kwamba unapaswa kufanya hivi kwa ajili yake, 5kwa sababu analipenda taifa letu, na ndiye aliyejenga sinagogi kwa ajili yetu”. 6Yesu akaendelea na safari yake pamoja nao. lakini kabla hajaenda mbali na nyumba, afisa mmoja aliwatuma marafiki zake kuzungumza naye. “Bwana, usijichoshe mwenyewe kwa sababu mimi sistahili wewe kuingia kwenye dari yangu. 7Kwa sababu hii sikufikiria hata mimi mwenyewe kuwa ninafaa kuja kwako, lakini sema neno tu na mtumishi wangu atapona. 8Kwani mimi pia ni mtu niliyewekwa kwenye mamlaka na nina askari chini yangu. Husema kwa huyu “Nenda” na huenda, na kwa mwingine, “Njoo” naye huja, na kwa mtumishi wangu 'Fanya hiki', na yeye hufanya”. 9Yesu aliposikia haya alishangaa, na kuwageukia makutano waliokuwa wanamfuata na kusema.”Nawaambia, hata katika Israeli, sijawahi kuona mtu mwenye imani kuu kama huyu. 10Kisha wale waliokuwa wametumwa walirudi nyumbani na kumkuta mtumishi akiwa mzima.
Watakatifu wa siku
- Mt. Yohane Krisostomo, askofu na mwalimu wa Kanisa
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki