Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Septemba 2027 › 6 Septemba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 6 Septemba 2027
Jumatatu · Juma la 23 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Jumatatu ya Juma la 23 la Mwaka
Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: kijani
Masomo ya siku
Somo la kwanza
24Sasa nafurahia mateso yangu kwa ajili yenu. Nami natimiliza katika mwili wangu kinachopungua kwa mateso ya Kristo kwa ajili ya mwili wake, ambao ni kanisa. 25Mimi ni mtumishi wa kanisa hili, sawasawa na wajibu niliopewa kutoka kwa Mungu kwa ajili yenu, kulijaza neno la Mungu. 26Huu ni ukweli wa siri iliyokuwa imefichwa kwa miaka mingi na kwa vizazi. Lakini sasa imefunuliwa kwa wote waaminio katika Yeye. 27Ni kwa wale ambao Mungu alitaka kufunua kulivyo utajiri wa utukufu wa siri ya ukweli huu miongoni mwa Mataifa. Ni kwamba Kristo yumo ndani yenu, ujasiri wa utukufu ujao. 28Huyu ndiye tunayemtangaza. Tunamwonya kila mtu, na kumfundisha kila mtu kwa hekima yote, ili kwamba tumlete kila mtu mkamilifu katika Kristo. 29Kwa jili hii, mimi najibidisha na kujitahidi kulingana na nguvu yake ifanyayo kazi ndani yangu katika uweza. 2:1Kwa kuwa nataka mfahamu jinsi ambavyo nimekuwa na taabu nyingi kwa ajili yenu, kwa wote walioko Laodikia na kwa wote ambao hawajaona uso wangu katika mwili. 2Nafanya kazi ili kwamba mioyo yao iweze kufarijiwa kwa kuletwa pamoja katika upendo na katika utajiri wote wa wingi wa uhakika kamili wa maarifa, katika kuijua siri ya kweli ya Mungu, ambaye ni Kristo. 3Katika Yeye hazina zote za hekima na maarifa zimefichwa.
Wimbo wa katikati
5Katika ukimya ninamsubiri Mungu pekee; kwa maana matumaini yangu yako kwake. 6Yeye pekee ni mwamba wangu na wokovu wangu; yeye ni mnara wangu mrefu; sitasogezwa. 8Mwaminini Mungu wakati wote, ninyi watu; mimina moyo wako mbele zake; Mungu ni kimbilio salama kwa ajili yetu. Selah
Injili
6Ilitokea katika Sabato nyingine kwamba alikwenda ndani ya sinagogi na kuwafundisha watu huko. Palikuwa na mtu ambaye mkono wake wa kulia ulikuwa umepooza. 7Waandishi na Mafarisayo walikuwa wanamwangalia kwa makini kuona kama angemponya mtu siku ya Sabato, ili waweze kupata sababu ya kumshtaki kwa kufanya kosa. 8Lakini alijua nini walikuwa wanafikiri na akasema kwa mtu aliyekuwa amepooza mkono, “Amka, simama hapa katikati ya kila mmoja.” Hivyo huyo mtu akanyanyuka na kusimama pale. 9Yesu akasema kwao, “Nawauliza ninyi, ni halali siku ya Sabato kufanya mema au kufanya madhara, kuokoa maisha au kuyaharibu?” Kisha aliwaangalia wote na kumwambia yule mtu, 10“Nyoosha mkono wako.” Akafanya hivyo, na mkono wake ulikuwa umeponywa. 11Lakini walijawa na hasira, wakaongeleshana wao kwa wao kuhusu nini wanapaswa wafanye kwa Yesu.
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki