Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Agosti 2027 › 3 Agosti
Kalenda ya Kiorthodoksi · 21 Julai (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 3 Agosti 2027
Jumanne · Wiki ya 7 baada ya Pentekoste · Sauti ya 5
Sikukuu na watakatifu
Nabii Ezekieli (karne ya 6 K.K.)
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
20Kwamba mlinunuliwa kwa thamani. Kwa hiyo mtukuzeni Mungu kwa miili yenu. 7:1Kuhusu mambo mliyoniandikia: Kuna wakati ambapo ni vizuri mwanaume asilale na mke wake. 2Lakini kwa sababu ya majaribu mengi ya zinaa kila mwanaume awe na mkewe, na kila mwanamke awe na mmewe. 3Mume anapaswa kumpa mke haki yake ya ndoa, na vile vile mke naye kwa mmewe. 4Si mke aliye na mamlaka juu ya mwili wake, ni mme. Na vile vile, mme naye hana mamlaka juu ya mwili wake, bali mke anayo. 5Msinyimane mnapolala pamoja, isipokuwa mmekubaliana kwa muda maalum. Fanyeni hivyo ili kupata muda wa maombi. Kisha mnaweza kurudiana tena pamoja, Ili kwamba Shetani asije akawajaribu kwa kukosa kiasi. 6Lakini nasema haya mambo kwa hiari na si kama amri. 7Natamani kila mmoja angekuwa kama mimi nilivyo. Lakini kila mmoja ana karama yake kutoka kwa Mungu. Huyu ana karama hii, na yule ana karama ile. 8Kwa wasioolewa na wajane ninasema kwamba, ni vizuri kwao kama wakibaki bila kuolewa, kama nilivyo mimi. 9Lakini kama hawawezi kujizuia, wanapaswa kuolewa. Kwa kuwa heri kwao kuolewa kuliko kuwaka tamaa. 10Sasa kwa wale walioolewa nawapa amri, si mimi bali ni Bwana. “Mke asitengane na mme wake.” 11Lakini kama akijitenga kutoka kwa mmewe, abaki hivyo bila kuolewa au vinginevyo apatane na mmewe. Na “Mme asimpe talaka mke wake.” 12Lakini kwa waliobaki, nasema- mimi, si Bwana- kwamba kama ndugu yeyote ana mke asiyeamini na anaridhika kuishi naye, hapaswi kumwacha.
Injili
1Kwa wakati huo, Herode alisikia habari juu ya Yesu.. 2Akawaambia watumishi wake, “Huyu ni Yohana Mbatizaji amefufuka kutoka katika wafu. Kwa hiyo nguvu hizi zipo juu yake.” 3Kwa kuwa Herode alikuwa amemkamata Yohana akamfunga na kumtupa gerezani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo kaka yake. 4Kwa kuwa Yohana alimwambia, “Si halali kumchukua yeye kuwa mke wake.” 5Herode angemwua lakini aliwaogopa watu kwa sababu walimwona Yohana kuwa nabii. 6Lakini wakati siku ya kuzaliwa Herode ilipofika binti wa Herodia alicheza katikati ya watu na kumpendeza Herode. 7Katika kujibu kili aliahidi kwa kiapo kwamba atampa chochote atakachoomba. 8Baada ya kushauriwa na mama yake, alisema, “Nipe mimi hapa katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji.” 9Mfalme alikuwa na sikitiko kwa maombi ya binti, lakini kwa ajili ya kiapo chake, kwa sababu ya wote waliokuwa chakulani pamoja naye aliamuru kwamba inapaswa ifanyike. 10Alituma Yohana aletwe kutoka gerezani 11ili akatwe kichwa chake na kikaletwa juu ya sinia na akapewa binti na akakipeleka kwa mama yake. 12Kisha wanafunzi wake wakaja kuuchukua ule mwili na kuuzika, baada ya hili walienda kumwambia Yesu. 13Naye Yesu aliposika haya, akijatenga kutoka mahali pale akapanda ndani ya mashuka akaenda sehemu iliyotengwa. Wakati umati ulipo fahamu alikokuwa, walimfuata kwa miguu kutoka mijini.
Watakatifu wa siku
- Watakatifu Watawa Simeoni, mjinga kwa ajili ya Kristo, na Yohana, mfungaji mwenzake (karibu 590)
- Mfiadini wa Kikasisi Petro, padri (1938)
- Kupatikana kwa masalia ya Binti wa Mfalme Mwaminifu Ana wa Kashin (1649)
- Watakatifu Watawa Onufrio, mnyamavu, na Onesimo, mtawa wa faragha, wa Mapango ya Kyiv (karne ya 12-13)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 21 Julai katika kalenda ya kanisa ni 3 Agosti katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki