Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Julai 2027 › 15 Julai

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 15 Julai 2027

Alhamisi · Juma la 15 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Alhamisi ya Juma la 15 la Mwaka

Kumbukumbu · Rangi ya liturujia: nyeupe

Mt. Bonaventura, askofu na mwalimu wa Kanisa · Kumbukumbu

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Kut 3:13–20

13Musa akamwambia Mungu, “Nikienda kwa Waisraeli na kuwaambia, 'Mungu wa baba zenu amenituma mimi kwenu,' na kisha wakiniambia, 'jina lake nani?' nitawaambia nini?” 14Mungu akamwambia Musa, “MIMI NIPO AMBAYE NIPO.” Mungu akasema, “Ni lazima uwaambie Waisraeli, “MIMI NIPO amenituma kwenu.” 15Pia Mungu akamwambia Musa, “Lazima uwaambie Waisraeli, 'Yahwe, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo amenituma mimi kwenu. Hili ndio jina langu milele, na hivi ndivyo nitakavyokumbukwa na vizazi vyote.' 16Nenda ukawakusanye wazee wa Israeli pamoja. Waambie, 'Yahwe, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Abrahamu, wa Isaka na Yakobo, amenitokea mimi na kusema, “Hakika nimewatazama na nimeona yale mliyotendewa huko Misri. 17Nimeahidi kuwatoa ninyi katika mateso ya Misri na kuwaleta katika nchi ya Wakanaani, Wahiti, Wamwori, Waperizi, Wahivi, na Wayebusi. Nchi ijaayo maziwa na asali.” 18Watakusikiliza. Wewe pamoja na wazee wa Israeeli itawapasa kwenda kwa mfalme wa Misri, na imewapasa kumwambia, 'Yahwe, Mungu wa Waebrania amekutana nasi. Hivyo tuache sisi twende safari ya siku tatu katika jangwa ili tupate kutoa sadaka kwa Yahwe Mungu wetu.' 19Lakini nafahamu ya kuwa mfalme wa Misri hatawaacha ninyi mwende, isipokuwa kwa kulazimishwa. 20Nitainua mkono wangu na kuwapiga Wamisri kwa miujiza yote nitakayoifanya kati yao. Baada ya hayo, atawaacha mwende.

Wimbo wa katikati

Zab 105:1, 5, 8–9, 24–27

1Mshukuruni Yahwe, liitieni jina lake; myafanye matendo yake yajulikane kati ya mataifa. 5Kumbukeni mambo ya ajabu aliyoyatenda, 8Naye hulikumbuka agano lake milele, neno alilo amuru kwa ajili ya vizazi elfu. 9Hulikumbuka agano alilolifanya na Ibrahimu na kiapo alicho mwapia Isaka. 24Yahwe aliwajalia watu wake wazae sana, na aliwafanya wenye nguvu kuliko adui zao. 25Alisababisha adui zao wawachukie watu wake, na kuwatendea visivyo watumishi wake. 26Alimtuma Musa, mtumishi wake, na Haruni, ambaye alikwisha mchagua. 27Walifanya ishara zake kati ya Wamisri na maajabu yake katika ya nchi ya Hamu.

Injili

Mt 11:28–30

28Njoni kwangu, nyinyi nyote mnaosumbuka na mnaolemewa na mzigo mzito, nami nitawapumzisha. 29Jitieni nira yangu na mjifunze kutoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mnyenyekevu na mpole wa moyo na mtapata pumziko la nafsi zenu. 30Kwa kuwa nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 15 Julai

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki