Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Julai 2027 › 11 Julai
Kalenda ya Kiorthodoksi · 28 Juni (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 11 Julai 2027
Jumapili · Sauti ya 2
Sikukuu na watakatifu
Jumapili ya 3 baada ya Pentekoste
Mfungo wa Mitume
Samaki wanaruhusiwa
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Injili ya 3 ya Sala ya Alfajiri
9Mapema katika siku ya kwanza ya juma, baada ya kufufuka, alimtokea kwanza Mariamu Magdalena, ambaye kutoka kwake alimtoa mapepo saba. 10Aliondoka na kuwaambia wale ambao walikuwa pamoja naye, wakati walipokuwa wakihuzunika na kutoa machozi. 11Walisikia kwamba ni mzima na ameonekana naye, lakini hawakumwamini. 12Baada ya hayo, akajitokeza katika namna tofauti kwa watu wengine wawili, wakati walipokuwa wakitembea kutoka katika nchi. 13Walienda na kuwaambia wanafunzi wengine waliobaki, lakini hawakuwaamini. 14Yesu baadaye akajitokeza kwa wale kumi na mmoja walipokuwa wameegama katika meza, na akawakemea kwa kutokuamini kwao na ugumu wa mioyo, kwa sababu hawakuwaamini wale waliomwona baada ya kufufuka kutoka kwa wafu. 15Akawaambia, “ Enendeni ulimwenguni mwote, na kuhubiri injili kwa viumbe vyote. 16Yeyote aaminiye na kubatizwa ataokolewa, na yule asiyeamini atahukumiwa. 17Ishara hizi zitaambatana na wote waaminio. Kwa jina langu watatoa pepo. Watasema kwa lugha mpya. 18Watashika nyoka kwa mikono yao, na hata wakinywa kitu chochote cha kufisha hakitawadhuru. Wataweka mikono kwa wagonjwa, nao watakuwa wazima”. 19Baada ya Bwana kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni na ameketi mkono wa kuume wa Mungu. 20Wanafunzi wakaondoka na kuhubiri kila mahali, wakati Bwana akifanya kazi nao na kulithibitisha neno kwa miujiza na ishara zikifuatana nao.
Waraka
1Kwa kuwa tumehesabiwa haki kwa njia ya imani, tuna amani na Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo. 2Kupitia yeye sisi pia tuna fursa kwa njia ya imani katika neema hii ambayo ndani yake tunasimama. Tunafurahi katika ujasiri atupao Mungu kwa ajili ya baadaye, ujasiri ambao tutashiriki katika utukufu wa Mungu. 3Siyo hili tu, lakini pia tunafurahi katika mateso yetu. Tunajua kwamba mateso huzaa uvumilivu. 4Uvumilivu huzaa kukubalika, na kukubalika huzaa ujasiri kwa ajili ya baadaye. 5Ujasiri huu haukatishi tamaa, kwa sababu upendo wa Mungu umemwagwa katika mioyo yetu kupitia Roho Mtakatifu, ambaye alitolewa kwetu. 6Kwa tulipokuwa tungali tu dhaifu, kwa wakati muafaka Kristo alikufa kwa ajili ya waovu. 7Kwa kuwa itakuwa vigumu mmoja kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki. Hii ni kwamba, pengine mtu angethubutu kufa kwa ajili ya mtu mwema. 8Lakini Mungu amehakikisha upendo wake mwenyewe kwetu, kwa sababu wakati tulipokuwa tungali wenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu. 9Kisha zaidi ya yote, sasa kwa kuwa tumehesabiwa haki kwa damu yake, tutaokolewa kwa hiyo kutoka katika gadhabu ya Mungu. 10Kwa kuwa, ikiwa wakati tulipokuwa maadui, tulipatanishwa na Mungu kwa njia ya kifo cha mwanae, zaidi sana, baada ya kuwa tumekwisha patanishwa, tutaokolewa kwa maisha yake.
Injili
22Jicho ni taa ya mwili. Kwa hiyo, ikiwa jicho lako ni zima, mwili wote utajazwa na nuru. 23Lakini ikiwa jicho lako ni bovu, mwili wako wote umejaa giza totoro. Kwahiyo, ikiwa nuru ambayo imo ndani yako ni giza hasa, ni giza kubwa kiasi gani! 24Hakuna hata mmoja anayeweza kuwatumikia mabwana wawili, kwa kuwa atamchukia mmoja na kumpenda mwingine, au la sivyo atajitoa kwa mmoja na kumdharau mwingine. Hamuwezi kumtumikia Mungu na mali. 25Kwa hiyo nakuambia, usiwe na mashaka kuhusu maisha yako, kuwa utakula nini au utakunywa nini, au kuhusu mwili wako, utavaa nini. Je! Maisha si zaidi ya chakula na mwili zaidi ya mavazi? 26Tazama ndege walioko angani. Hawapandi na hawavuni na hawakusanyi na kutunza ghalani, lakini Baba yenu wa mbinguni huwalisha wao. Je ninyi si wa thamani zaidi kuliko wao? 27Na ni nani miongoni mwenu kwa kujihangaisha anaweza kuongeza dhiraa moja kwenye uhai wa maisha yake? 28Na kwa nini mna kuwa na wasiwasi kuhusu mavazi? Fikiria kuhusu maua kwenye mashamba, jinsi yanavyokua. Hayafanyi kazi na hayawezi kujivisha. 29Bado ninawaambia, hata Sulemani katika utukufu wake wote hakuvikwa kama mojawapo ya haya. 30Ikiwa Mungu anayavalisha majani katika mashamba, ambayo yadumu siku moja na kesho yanatupwa katika moto, je ni kwa kiasi gani atawavalisha ninyi, ninyi wenye imani ndogo? 31Kwa hiyo msiwe na wasiwasi nakusema, 'Je tutakula nini?' au “Je tutakunywa nini?” au “Je tutavaa nguo gani?” 32Kwa kuwa mataifa wanatafuta mambo haya, na Baba yenu wa mbinguni anajua kuwa mnahitaji hayo. 33Lakini kwanza tafuteni ufalme wake na haki yake na haya yote yatakabidhiwa kwako.
Watakatifu wa siku
- Kuhamishwa kwa masalia ya Wafiadini Kiro na Yohana, matabibu wasiopokea malipo na watenda miujiza (412)
- Watakatifu Watawa Sergio na Germano, watenda miujiza wa Valaam (karne ya 14)
- Mfiadini wa Kikasisi Basili, shemasi (1918)
- Mtawa Mfiadini Sebastiana (1938)
- Mfiadini wa Kikasisi Gregori, shemasi (1940)
- Mtakatifu Mtawa Ksenofoni wa Robeika (1262)
- Mtakatifu Mtawa Paulo, tabibu
- Ikoni ya Mama wa Mungu iitwayo “Mwenye Mikono Mitatu” (karne ya 8)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 28 Juni katika kalenda ya kanisa ni 11 Julai katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki