Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Julai 2027 › 9 Julai
Kalenda ya Kiorthodoksi · 26 Juni (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 9 Julai 2027
Ijumaa · Wiki ya 3 baada ya Pentekoste · Sauti ya 1
Sikukuu na watakatifu
Mtakatifu Mtawa Daudi wa Thesalonike (karne ya 6)
Mfungo wa Mitume
Mfungo: pamoja na mafuta
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
6Lakini si kwamba ahadi za Mungu zimeshindwa kutimia. Maana si kila mtu aliye Israeli ni Mwiisraeli halisi. 7Sivyo hata kwa uzao wa Abrahamu kuwa ni watoto wake halisi. Lakini, “ni kupitia Isaka uzao wako utaitwa.” 8Hii ni kwamba, watoto wa mwili si watoto wa Mungu. Lakini watoto wa ahadi wanatazamwa kuwa kama uzao. 9Maana hili ndilo neno la ahadi: “Katika majira haya nitakuja, na Sara atapewa mtoto.” 10Si hili tu, lakini baada ya Rebeka kupata mimba kwa mtu mmoja, Isaka baba yetu- 11kwamba watoto walikuwa bado hawajazaliwa na alikuwa hajafanya jambo lolote zuri au baya, ili kwamba kusudi la Mungu kulingana na uchaguzi lisimame, wala si kwa matendo, lakini ni kwa sababu ya yule aitae. 12Ilinenwa kwake, “Mkubwa atamtumikia mdogo.” 13Kama ilivyo kwisha andikwa: “Yakobo nilimpenda, lakini Esau nilimchukia.” 14Basi tena tutasema nini? Je kuna udhalimu kwa Mungu? La hasha. 15Kwa kuwa anasema kwa Musa, “nitakuwa na rehema kwa yule nitakayemrehemu, na nitakuwa na huruma kwa yule nitakayemhurumia.” 16Kwa hiyo basi, si kwa sababu ya yeye atakaye, wala si kwa sababu ya yeye ambaye hukimbia, lakini kwa sababu ya Mungu, ambaye huonesha rehema. 17Kwa kuwa maandiko husema kwa Farao, “Kwa kusudi hili maalumu nilikuinua, ili kwamba nioneshe nguvu zangu katika wewe, na ili kwamba jina langu litangazwe katika nchi yote.” 18Hivyo basi, Mungu huwa na rehema kwa yeyote ampendaye, na kwa ambaye humpenda, humfanya kuwa mkaidi. 19Kisha utasema kwangu, “Kwa nini bado anaona kosa? Ni yupi ambaye alikwisha kustahimili matakwa yake?”
Injili
32Hivyo basi kila mmoja atakaye nikiri mbele za watu, nami pia nitamkiri mbele ya Baba yangu aliye mbinguni. 33Lakini yeye atakaye nikana mbele za watu, nami pia nitamkana mbele ya Baba yangu aliye mbinguni. 34Msifikiri kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani, lakini upanga. 35Kwa kuwa nilikuja kumweka mtu apingane na baba yake, na binti dhidi ya mama yake, na mkwe dhidi ya mama mkwe wake. 36Adui wa mtu watakuwa wale wa nyumbani mwake. 11:1Ikawa baada ya Yesu kumaliza kuwaelekeza wanafunzi wake kumi na wawili aliondoka plae kwenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao,
Watakatifu wa siku
- Ikoni ya Mama wa Mungu ya Tikhvin (1383)
- Mfiadini wa Kikasisi Georgi, padri (1918)
- Mtakatifu Mtawa Yohana, Askofu wa Wagothi († 790)
- Askofu Mtakatifu Dionisio, Askofu Mkuu wa Suzdal (1385)
- Kupatikana kwa masalia ya Mtakatifu Mtawa Tikhon wa Lukh, wa Kostroma (1569)
- Ikoni za Mama wa Mungu za Lida (ya Roma) (karne ya 1), za Neamț (1399) na za Maziwa Saba (karne ya 17)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 26 Juni katika kalenda ya kanisa ni 9 Julai katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki