Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Juni 2027 › 28 Juni
Kalenda ya Kiorthodoksi · 15 Juni (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 28 Juni 2027
Jumatatu · Wiki ya 2 baada ya Pentekoste · Sauti ya 8
Sikukuu na watakatifu
Nabii Amosi (karne ya 8 K.K.)
Mfungo wa Mitume
Samaki wanaruhusiwa
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
28Kwa maana yeye si Myahudi aliye kwa hali ya nje; wala kutahiriwa si kule ambako ni kwa nje tu katika mwili. 29Lakini yeye ni Myahudi aliye kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko. Sifa ya mtu wa namna hiyo haitokani na watu bali yatoka kwa Mungu. 3:1Kisha ni faida gani aliyo nayo Myahudi? Na faida ya tohara ni nini? 2Ni vyema sana kwa kila njia. Awali ya yote, Wayahudi walikabidhiwa ufunuo kutoka kwa Mungu. 3Lakini, itakuwaje iwapo baadhi ya Wayahudi hawakuwa na imani? Je, kutokuamini kwao kutafanya uaminifu wa Mungu kuwa batili? 4La hasha. Badala yake, acha Mungu aonekane kuwa kweli, hata kama kila mtu ni mwongo. Kama ilivyokuwa imeandikwa, “Ya kwamba uweze kuonekana kuwa mwenye haki katika maneno yako, na uweze kushinda uingiapo katika hukumu.” 5Lakini ikiwa uovu wetu unaonesha haki ya Mungu, tuseme nini? Mungu si dhalimu atoapo ghadhabu yake, je yupo hivyo? Naongea kutokana na mantiki ya kibinadamu. 6La hasha! Ni jinsi gani basi Mungu atauhukumu ulimwengu? 7Lakini ikiwa kweli ya Mungu kupitia uongo wangu hutoa sifa tele kwa ajili yake, kwa nini ningali bado nahukumiwa kama mwenye dhambi? 8Kwa nini tusiseme, kama tulivyosingiziwa na kama wengine wanavyothibitisha kwamba tunasema, “Tufanye uovu, ili mema yaje”? Hukumu juu yao ni ya haki. 9Ni nini basi? Tunajitetea wenyewe? Hapana kabisa. Kwa kuwa sisi tayari tumewatuhumu Wayahudi na Wayunani wote pamoja, ya kuwa wapo chini ya dhambi. 10Hii ni kama ilivyoandikwa: “Hakuna mwenye haki, hata mmoja. 11Hakuna mtu ambaye anaelewa. Hakuna mtu ambaye anamtafuta Mungu. 12Wote wamegeuka. Wao kwa pamoja wamekuwa hawana maana. Hakuna atendaye mema, la, hata mmoja. 13Makoo yao ni kaburi lililo wazi. Ndimi zao zimedanganya. Sumu ya nyoka ipo chini ya midomo yao. 14Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu. 15Miguu yao ina mbio kumwaga damu. 16Uharibifu na mateso yapo katika njia zao. 17Watu hawa hawajajua njia ya amani. 18Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yao.”
Injili
31Kwa hiyo msiwe na wasiwasi nakusema, 'Je tutakula nini?' au “Je tutakunywa nini?” au “Je tutavaa nguo gani?” 32Kwa kuwa mataifa wanatafuta mambo haya, na Baba yenu wa mbinguni anajua kuwa mnahitaji hayo. 33Lakini kwanza tafuteni ufalme wake na haki yake na haya yote yatakabidhiwa kwako. 34Kwa hiyo, usione shaka kwa ajili ya kesho, kwa kuwa kesho itajishughulikia yenyewe. Kila siku inatosha kuwa na tatizo lake yenyewe. 7:9Au kuna mtu miongoni mwenu ambaye, ikiwa mtoto wake amemwomba kipande cha mkate atampa jiwe? 10Au ikiwa atamwomba samaki, na yeye atampa nyoka? 11Kwa hiyo, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, Je! Ni kiasi gani zaidi Baba aliye mbinguni atawapa vitu vizuri wale wanao muomba yeye?
Watakatifu wa siku
- Askofu Mtakatifu Yona, Mitropoliti wa Moscow na Urusi yote, mtenda miujiza († 1461)
- Mfiadini wa Kikasisi Amosi, padri (1919)
- Wafiadini Vito, Modesto na Kreskentia († karibu 303)
- Mfiadini Dula wa Kilikia (karibu 305-313)
- Mbarikiwa Yeronimo wa Stridon (419-420)
- Mbarikiwa Augustino, Askofu wa Hippo (430)
- Kuhamishwa kwa masalia ya Mtakatifu Mtawa Theodoro wa Sikeoni, Askofu wa Anastasiopoli († karibu karne ya 9)
- Mfiadini Lazar, Mwana wa Mfalme Mwaminifu wa Serbia (1389)
- Askofu Mtakatifu Efraimu II, Patriarki wa Serbia (baada ya 1399)
- Kupatikana kwa masalia ya Watawa Wafiadini Gregori na Kasiani wa Avnega (1524)
- Mtakatifu Mtawa Dula, mvumilivu wa mateso, wa Misri
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 15 Juni katika kalenda ya kanisa ni 28 Juni katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki