Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Juni 2027 › 12 Juni

Kalenda ya Kiorthodoksi · 30 Mei (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 12 Juni 2027

Jumamosi · Wiki ya 6 ya Pasaka · Sauti ya 5

Sikukuu na watakatifu

Mtakatifu Mtawa Isaka wa Dalmato († 383)

Mfungo

Hakuna mfungo

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Waraka

Mdo 20:7–12

7Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekusanyika pamoja ili kuumega mkate, Paulo alizungumza na Waamini. Alikuwa akipanga kuondoka kesho yake, hivyo akaendelea kuongea hadi usiku wa manane. 8Kulikuwa na taa nyingi katika chumba cha juu ambapo tulikuwa tumekusanyika pamoja. 9Katika dirisha alikuwa amekaa kijana mmoja jina lake Utiko, ambaye alielemewa na usingizi mzito. Hata Paulo alipokuwa akihutubu kwa muda mrefu, kijana huyu, akiwa amelala, akaanguka chini kutoka ghorofa ya tatu na aliokotwa akiwa amekufa. 10Lakini Paulo alishuka chini, alijinyoosha yeye mwenyewe juu yake, akamkumbatia. Kisha akasema, “Msikate tamaa, kwa kuwa yu hai.” 11Kisha akapanda tena ghorofani na akaumega mkate, akala. Baada ya kuzungumza nao kwa muda mrefu hadi alfajiri, akaondoka. 12Wakamleta yule kijana akiwa hai wakafarijika sana.

Injili

Yn 14:10–21

10Hamuamini kuwa mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Maneno ninayoyasema kwenu sisemi kwa kusudi langu mwenyewe; badala yake, ni Baba anayeishi ndani yangu anayetenda kazi yake. 11Niamini mimi, kwamba niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani yangu; kadhalika niamini mimi kwa sababu ya kazi zangu hasa. 12Amini, amini, nawaambia, yeye aniaminiye, mimi kazi zile nizifanyazo, atazifanya kazi hizi pia; na atafanya hata kazi kubwa kwasababu ninakwenda kwa Baba. 13Chochote mkiomba katika jina langu, nitafanya ili kwamba Baba aweze kutukuzwa katika Mwana. 14Kama mkiomba kitu chochote katika jina langu, hilo nitafanya. 15Kama mkinipenda, mtazishika amri zangu. 16Na nitamwomba Baba, Naye atawapa Msaidizi mwingine ili kwamba aweze kuwa pamoja nanyi milele, 17Roho wa kweli. Ulimwengu hauwezi kumpokea yeye kwa sababu haumuoni, au kumjwa yeye. hata hivyo ninyi, mnamjua yeye, kwani anakaa pamoja nayi na atakuwa ndani yenu. 18Sitawaacha peke yenu; Nitarudi kwenu. 19Kwa muda kitambo, ulimwengu hautaniona tena, lakini ninyi mwaniona. Kwa sababu ninaishi, nanyi mtaishi pia. 20Katika siku hiyo mtajua kwamba mimi niko ndani ya Baba, na kwamba ninyi mko ndani yangu, na kwamba mimi niko ndani yenu. 21Yeyote azishikaye amri zangu na kuzitenda, ndiye mmoja ambaye anipenda mimi; na ambaye anipenda mimi atapendwa na Baba yangu, na Nitampenda na nitajionyesha mimi mwenyewe kwake.”

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 12 Juni

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 30 Mei katika kalenda ya kanisa ni 12 Juni katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki