Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Mei 2027 › 14 Mei

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 14 Mei 2027

Ijumaa · Juma la 7 la Pasaka

Sikukuu na watakatifu

Mt. Mathia, mtume

Sikukuu · Rangi ya liturujia: nyekundu

Kufunga na toba

Siku ya toba

Kila Ijumaa ni siku ya toba; kila baraza la maaskofu huamua jinsi inavyoadhimishwa: kujinyima nyama au tendo lingine la toba. Kufunga kunawahusu wenye miaka 18 hadi 59, kujinyima nyama kuanzia miaka 14.

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Mdo 1:15–17, 20–26

15Katika siku zile Petro alisimama katikati ya ndugu, kama watu 120, akasema, 16Ndugu, ilikuwa lazima kwamba maandiko yatimizwe, ambapo zamani Roho Mtakatifu alisema kwa kinywa cha Daudi kuhusiana na Yuda, ambaye aliwaelekeza wale waliomkamata Yesu. 17Kwa kuwa yeye alikuwa mmoja wetu na alipokea fungu lake la faida katika hii huduma.” 20“Kwenye kitabu cha Zaburi imeandikwa, 'Ngoja eneo lake liwe hame na isiruhusiwe hata mmoja kuishi pale;' na, 'Ruhusu mtu mwingine achukue nafasi yake ya uongozi.' 21Hiyo ni muhimu, kwa hiyo, mmoja wa wanaume ambao waliambatana nasi wakati Bwana Yesu alipotoka na kuingia kati yetu, 22kuanzia kwenye ubatizo wa Yohana mpaka siku ile alipotwaliwa juu, lazima awe shahidi wa ufufuo pamoja nasi. 23“Wakaweka mbele wanaume wawili, Yusufu aitwaye Barnaba, ambaye pia aliitwa Yusto na Mathia. 24Wao waliomba wakisema, “Wewe, Bwana, ujuaye mioyo ya watu wote, hivyo weka wazi yupi kati ya wawili hawa ambaye umemchagua 25kuchukua nafasi katika huduma na utume, ambapo Yuda alitenda uovu na kwenda mahali pake.” 26Wakapiga kura kwa ajili yao, na kura ikamwangukia Mathia ambaye alihesabiwa pamoja na wale mitume kumi na moja.

Wimbo wa katikati

Zab 113:1–8

1Msifuni Yahwe. Msifuni yeye, enyi watumishi wa Yahwe; lisifuni jina la Yahwe. 2Litukuzwe jina la Yahwe, tangu sasa na hata milele. 3Toka maawio ya jua hata machweo yake, Jina la Yahwe lazima lisifiwe. 4Yahwe ameinuliwa juu ya mataifa yote, na utukufu wake wafika juu mbinguni. 5Ni nani aliye kama Yahwe Mungu wetu, aliye na kiti chake juu, 6atazamaye chini angani na duniani? 7Humwinua maskini toka mavumbini na kumpandisha muhitaji kutoka jaani, 8ili amketishe pamoja na wakuu, pamoja na wakuu wa watu wake.

Injili

Yn 15:9–17

9Kama baba yangu alivyonipenda mimi, mimi pia nimewapenda ninyi; dumuni katika pendo langu. 10Ikiwa mtashika amri zangu, mtadumu katika pendo langu kama nilivyo shika amri za baba yangu na kudumu katika pendo lake. 11Nimesema mambo haya kwenu ili kwamba furaha yangu iwe ndani yenu na ili kwamba furaha yenu ifanyike kuwa timilifu. 12Hii ndiyo amri yangu, kwamba mpendane ninyi kwa ninyi kama nilivyo wapenda ninyi. 13Hakuna mtu aliye na upendo mkuu kuliko huu, kwamba ayatoe maisha yake kwa ajiliya rafiki zake. 14Ninyi ni rafiki zangu ikiwa mtafanya yale niwaagizayo. 15Siwaiti watumwa, kwa kuwa mtumwa hajui kile afanyacho bwana wake. Nimewaita ninyi marafiki, kwa sababu nimewajulisheni mambo yote ambayo nimesikia kutoka kwa Baba. 16Hamkunichagua mimi, bali mimi niliwachagua ninyi na kuwaweka mwende mazae matunda, na tunda lenu lipate kukaa. Hii liko hivi ili kwamba chochote muombacho kwa Baba kwa jina langu, atawapeni. 17Mambo haya ninawaagiza, kwamba mpendane kila mtu na mwenzake.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 14 Mei

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki