Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Machi 2027 › 28 Machi
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 28 Machi 2027
Jumapili · Oktava ya Pasaka
Sikukuu na watakatifu
Dominika ya Pasaka: Ufufuko wa Bwana
Sherehe · Rangi ya liturujia: nyeupe
Masomo ya siku
Somo la kwanza
34Ndipo Petro akafungua mdomo wake na kusema “Kweli, nimeamini kuwa Mungu hawezi kuwa na upendeleo. 37ninyi wenyewe mnajua tukio lililotokea, ambalo limetokea Yudea yote na lilianzia Galilaya, baada ya ubatizo ambao Yohana alitangaza. 38tukio lililokuwa linamhusu Yesu Kristo jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na kwa nguvu. Alienda akifanya mema na kuponya wote walioteswa na ibilsi, kwa kuwa Mungu alikuwa pamoja naye. 39Sisi ni mashahidi wa mambo yote aliyoyafanya katika nchi za Uyahudi na katika Yerusalemu- huyu ni Yesu waliyemuua na kumtundika mtini. 40Huyu mtu Mungu alimfufua siku ya tatu na kumpa kujulikana, 41si kwa watu wote, lakini kwa mashahidi waliochaguliwa kabla na Mungu. - sisi wenyewe, tulio kula naye na kunywa naye baada ya kufufuka kutoka kwa wafu. 42Ametuagiza kuhubiri kwa watu na kushuhudia kuwa huyu ndiye ambaye Mungu alimchagua kuwa mwamuzi wa walio hai na waliokufa. 43Katika yeye manabii wote washuhudie, ili kwamba kila anayeamini katika yeye atapokea msamaha wa dhambi kupitia jina lake.”
Wimbo wa katikati
1Mshukuruni Yahwe, kwa kuwa ni mwema, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele. 2Israeli na aseme, “Uaminifu wa agano lake wadumu milele.” 16Mkono wa kuume wa Mungu umetukuka; mkono wa kuume wa Yahwe umeshinda. 17Sitakufa, bali nitaishi na kuyatangaza matendo ya Yahwe. 22Jiwe ambalo wajenzi walilikataa wajenzi limekuwa msingi. 23Yahwe ndiye afanyaye hili; ni la ajabu machoni petu.
Somo la pili
au: 1 Kor 5:6–8
1Ikiwa tena Mungu amewafufua pamoja na Kristo, yatafuteni mambo ya juu ambako Kristo anakaa mkono wa kuume wa Mungu. 2Fikirini kuhusu mambo ya juu, sio kuhusu mambo ya duniani. 3Kwa kuwa mmekufa, na maisha yenu yamefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. 4Wakati Kristo atakapoonekana, ambaye ni maisha yenu, ndipo nanyi pia mtaonekana naye katika utukufu.
Injili
1Mapema siku ya kwanza ya juma, kungali bado giza, Mariamu Magdalena alikuja kaburini; akaliona lile jiwe limeondolewa kaburini. 2Kwa hiyo akakimbia mbio kwenda kwa Simon Petro na kwa yule mwanafunzi mwingine ambaye Yesu alimpenda, kisha akawaambia, “wamemchukua Bwana kaburini, nasi hatujui kule walikomlaza.” 3Kisha Petro na yule mwanafunzi mwingine wakatoka, kuelekea kaburini. 4Wote walipiga mbio kwa pamoja; yule mwanafunzi mwingine alikimbia kwa kasi zaidi ya Petro nakufika kaburini wa kwanza. 5Akasimama na kisha kuangalia kaburini; akaiona ile sanda ya kitani imelala, lakini hakuingia ndani. 6Kisha Simon Petro naye akafika akaingia ndani ya Kaburi. Akaiona ile sanda ya kitani imelala pale 7na ile leso iliyokuwa kichwani pake haikuwa imelala pamoja na zile sanda za kitani bali ilikuwa imelala pembeni peke yake. 8Ndipo yule mwanafunzi mwingine naye alipoingia ndani ya kaburi; akaona na kuamini. 9Kwa kuwa hadi wakati huo walikuwa bado hawajayajua maandiko kwamba ilimlazimu Yesu afufuke tena katika wafu.
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki