Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Februari 2027 › 10 Februari
Kalenda ya Kiorthodoksi · 28 Januari (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 10 Februari 2027
Jumatano · Wiki ya 37 baada ya Pentekoste · Sauti ya 3
Sikukuu na watakatifu
Mtakatifu Mtawa Efraimu Mshami (373-379)
Siku ya mfungo
Samaki wanaruhusiwa
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
11Je, kisima kimoja huweza kutoa maji matamu na machungu? 12Ndugu zangu, Je, mti wa mtini unaweza kuzaa matunda ya mzeituni, au mzabibu unazaa matunda ya mtini? Wala chemchemi ya maji chumvi haitoi maji yasio na chumvi. 13Ni nani miongoni mwenu aliye na hekima na ufahamu? Hebu mtu huyo na aoneshe maisha mema katika kazi zake kwa unyenyekevu utokanao na hekima. 14Lakini kama mnao wivu mkali na nia ya ubinafsi mioyoni mwenu, msijivune na kusema uongo mkiupinga ukweli. 15Hii siyo hekima ile ishukayo kutoka juu, lakini badala yake ni ya kidunia, si ya kiroho, na ni ya kipepo. 16Kwa kuwa palipo na wivu na ubinafsi upo, kuna vurugu na kila matendo maovu 17Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, kisha kupenda amani, upole na ukarimu, yenye kujaa rehema na matunda mema, bila kupendelea watu fulani, na kweli. 18Na tunda la haki hupandwa katika amani kwa wale ambao wanatenda mambo ya amani. 4:1Ugonvi na migogoro miongoni mwenu vyatoka wapi? Haviinuki kutoka katika tamaa zenu mbaya zinazoleta vita ndani ya washirika wenu? 2Mnatamani kile msichokuwa nacho. Mnauwa na mnafukuzia kile msichoweza kuwa nacho. Mnapigana na kugombana, na bado hampati kwa sababu hamumwombi Mungu. 3Mnaomba na hampokei kwa sababu mnaomba kwa ajili ya mambo mabaya, ili kwamba muweze kuvitumia kwa tamaa zenu mbaya. 4Enyi wazinzi! Hamjui kwamba urafiki na ulimwengu ni uadui dhidi ya Mungu? Kwa hiyo, yeyote aamuaye kuwa rafiki wa ulimwengu hujifanya mwenyewe adui wa Mungu. 5Au mnadhani maandiko hayana maana yasemapo kwamba Roho aliyoweka ndani yetu ana wivu sana kwa ajili yetu? 6Lakini Mungu hutoa neema zaidi, ndiyo maana maandiko husema, “Mungu humpinga mwenye kiburi, lakini humpa neema mnyenyekevu.”
Injili
23Amini nawaambia kwamba kila auambiaye mlima huu, 'Ondoka, na ukajitupe mwenyewe baharini, 'na kama hana mashaka moyoni mwake lakini anaamini kwamba alichokisema kitatokea, hivyo ndivyo Mungu atakavyofanya. 24Kwa hiyo ninawaambia: kila kitu muombacho na kuuliza kwa ajili yake, aminini kwamba mmepokea, navyo vitakuwa vyenu. 25Wakati mnaposimama na kuomba, mnapaswa kusamehe chochote mlichonacho dhidi ya yeyote, ili kwamba Baba yenu aliye mbinguni awasamehe pia ninyi makosa yenu.
Watakatifu wa siku
- Mtakatifu Mtawa Theodosio wa Totma (1568)
- Mtakatifu Theodoro Mwungamaji, padri (1933)
- Mfiadini wa Kikasisi Ignatio, Askofu wa Skopin (1938)
- Mfiadini wa Kikasisi Vladimir, padri, na Mtawa Mfiadini Bartholomayo (1938)
- Mfiadini Olga (1938)
- Mtakatifu Mtawa Leontio Mwungamaji (1972)
- Mtakatifu Mtawa Paladio, mkaa jangwani (karne ya 4)
- Mtakatifu Mtawa Isaka Mshami, Askofu wa Ninawi (karne ya 6-7)
- Mtakatifu Mtawa Efraimu wa Novy Torg (1053)
- Mtakatifu Mtawa Efraimu wa Mapango ya Kyiv, Askofu wa Pereyaslav (karibu 1098)
- Ikoni ya Mama wa Mungu ya Sumorin ya Totma (karne ya 16)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 28 Januari katika kalenda ya kanisa ni 10 Februari katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki