Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Januari 2027 › 20 Januari

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 20 Januari 2027

Jumatano · Juma la 2 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumatano ya Juma la 2 la Mwaka

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani

Mt. Fabiani, papa na shahidi · Kumbukumbu ya hiari

Mt. Sebastiani, shahidi · Kumbukumbu ya hiari

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Ebr 7:1–3, 15–17

1Ilikuwa hivi Melkizedeki, mfalme wa Salemu, Kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Abrahamu akirudi kutoka kuwaua wafalme na akambariki. 2Abrahamu alimpa moja ya kumi ya kila kitu alichokuwa amekiteka. Jina lake “Melkizedeki “ maana yake” mfalme wa haki” na pia “mflame wa Salemu” ambayo ni “mfalme wa amani.” 3Hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku wala mwisho wa maisha yake. Badala yake, anabakia kuhani milele, kama mwana wa Mungu. 15Na haya tusemayo ni wazi hasa ikiwa kuhani mwingine atatokea kwa mfano wa Melkizedeki. 16Kuhani huyu mpya siyo mmoja ambaye amekuwa kuhani juu ya msingi wa sheria zinazohusiana na uzao wa mtu, lakini katika msingi wa nguvu ya maisha yasiyoweza kuharibika. 17Hivyo maandiko yanashuhudia kuhusu yeye: “Wewe ni kuhani milele baada ya mfumo wa Melkizedeki.”

Wimbo wa katikati

Zab 110:1–4

1Zaburi ya Daudi. Yahwe humwambia bwana wangu, “Kaa mkono wangu wa kuume mpaka nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.” 2Yahwe atainyosha fimbo ya nguvu yako toka Sayuni; utawale kati ya adui zako. 3Siku ile ya uweza wako watu wako watakufuata wakiwa katika mavazi matakatifu ya hiari yao wenyewe; tokea tumbo la alfajiri ujana wako utakuwa kwako kama umande. 4Yahwe ameapa, na hatabadilika: “Wewe ni kuhani milele, baada ya namna ya Melkizedeki.”

Injili

Mk 3:1–6

1Na tena aliingia ndani ya sinagogi na mle palikuwa na mtu mwenye mkono uliopooza. 2Baadhi ya watu walikuwa wakimfuatilia kwa ukaribu kuona kama atamponya siku ya Sabato ili kwamba wamshitaki. 3Yesu alimwambia mtu mwenye mkono uliopooza, “ Inuka na usimame katikati ya umati huu.” 4Kisha akawaambia watu, “Je ni halali kutenda tendo jema siku ya Sabato au kutenda yasiyo haki; kuokoa maisha, au kuua?” Lakini walibaki kimya. 5Akawaangalia kwa hasira, akihuzunika kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao, na akamwambia yule mtu, “Nyoosha mkono wako”. Akaunyoosha na Yesu akamponya mkono wake. 6Mafarisayo wakaenda nje na mara wakafanya njama pamoja na Maherode dhidi yake ili kumuua.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 20 Januari

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki