Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Januari 2027 › 3 Januari
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 3 Januari 2027
Jumapili · Kipindi cha Noeli
Sikukuu na watakatifu
Dominika ya 2 baada ya Noeli
Dominika · Rangi ya liturujia: nyeupe
Jina Takatifu Kabisa la Yesu · Kumbukumbu ya hiari
Masomo ya siku
Somo la kwanza
Haimo katika tafsiri hii
Wimbo wa katikati
12Msifuni Yahwe, Yerusalemu, msifuni Mungu wenu, Sayuni. 13Maana yeye huyakaza mapingo ya malango yako, huwabariki watoto wako kati yako. 14Huletamafanikio ndani ya mipaka yako, hukutosheleza kwa ngano bora. 15Huipeleka amri yake juu ya nchi, amri zake hupiga mbio sana. 19Hutangaza neno lake kwa Yakobo, amri zake na hukumu zake kwa Israeli. 20Hajafanya hivyo kwa taifa linginelo lolote, na kama ilivyo amri zake, hawazijui. Msifuni Yahwe.
Somo la pili
3Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo apewe sifa. Ni yeye aliyetubariki kwa kila baraka za kiroho, katika mahali pa mbingu ndani ya Kristo. 4Kabla ya kuumbwa ulimwengu, Mungu alituchagua sisi ambao tunaamini katika Kristo. Alituchagua sisi ili tuweze kuwa watakatifu na tusiolaumika mbele yake. 5Katika pendo Mungu alituchagua mwanzo kwa kututwaa kama watoto wake kwa njia ya Yesu Kristo. Alifanya hivi kwa sababu alipendezwa kufanya kile alichotamani. 6Matokeo yake ni kwamba Mungu anatukuzwa kwa neema ya utukufu wake. Hiki ndicho alichotupatia bure kwa njia ya mpendwa wake. 15Kwa sababu hii, tangu wakati niliposikia kuhusu imani yenu ndani ya Bwana Yesu na kuhusu pendo lenu kwa wale wote ambao wametengwa kwa ajili yake. 16Sijaacha kumshukuru Mungu kwa ajili yenu na kuwataja katika maombi yangu. 17Ninaomba kwamba Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, baba wa utukufu, atawapeni roho ya hekima, mafunuo ya ufahamu wake. 18Ninaomba kwamba macho yenu ya moyoni yatiwe nuru kwa ninyi kujua ni upi ujasiri wa kuitwa kwenu. Naomba kwamba mjue utajiri wa utukufu wa urithi wake miongoni mwa wale waliotengwa kwa ajili yake.
Injili
1Mwanzoni kulikuwako Neno, na Neno alikuwa pamoja na Mungu, na Neno alikuwa Mungu. 2Huyu, Neno, Mwanzoni alikuwa pamoja na Mungu. 3Vitu vyote vilifanyika kupitia yeye, na pasipo yeye hakuna hata kitu kimoja kilichokuwa kimefanyika. 4Ndani yake kulikuwa uzima, na huo uzima ulikuwa nuru ya wanadamu wote. 5Nuru yang'aa gizani, wala giza halikuizimisha. 6Palikuwa na mtu aliyetumwa kutoka kwa Mungu, ambaye jina lake alikuwa Yohana. 7Alikuja kama shahidi kushuhudia kuhusu ile nuru, ili kwamba wote waweze kuamini kupitia yeye. 8Yohana hakuwa ile nuru, bali alikuja ili ashuhudie kuhusu ile nuru 9Hiyo ilikuwa nuru ya kweli ambayo ilikuwa inakuja katika dunia nayo humtia nuru kila mmoja 10Alikuwa katika dunia, na dunia iliumbwa kupitia yeye, na dunia haikumjua. 11Alikuja kwa vitu vyake, na watu wake hawakumpokea. 12Bali kwa wale wengi waliompokea, ambao waliamini jina lake, kwa hao aliwapa haki ya kuwa wana wa Mungu, 13Ambao walizaliwa, sio kwa damu, wala kwa mapenzi ya mwili, wala kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu mwenyewe. 14Naye Neno alifanyika mwili na akaishi miongoni mwetu, tumeuona utukufu wake, utukufu kama wa mtu pekee wa kipekee aliyekuja kutoka kwa Baba, amejaa neema na kweli. 15Yohana alishuhudia kuhusu yeye, na alipaza sauti akisema, “Huyu ndiye ambaye nilisema habari zake nikisema, “Yule ajaye baada yangu ni mkuu kuliko mimi, kwa sababu amekuwako kabla yangu.” 16Kwa kuwa kutoka katika utimilifu wake, sisi sote tumepokea bure kipawa baada ya kipawa. 17Kwa kuwa sheria ililetwa kupitia Musa. Neema na kweli vilikuja kupitia Yesu Kristo. 18Hakuna mwanadamu aliyemwona Mungu wakati wowote. Mtu pekee ambaye ni Mungu, aliye katika kifua cha Baba, amemfanya yeye ajulikane.
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki