Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Desemba 2026 › 18 Desemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 5 Desemba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 18 Desemba 2026
Ijumaa · Wiki ya 29 baada ya Pentekoste · Sauti ya 3
Sikukuu na watakatifu
Mtakatifu Mtawa Sava Aliyetakaswa (532)
Mfungo wa Kuzaliwa kwa Bwana
Mfungo: pamoja na mafuta
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Sala ya Jioni: somo
Haimo katika tafsiri hii
Sala ya Jioni: somo
Haimo katika tafsiri hii
Sala ya Jioni: somo
Haimo katika tafsiri hii
Sala ya Alfajiri: Injili
17Kisha Yesu alitelemka pamoja nao toka mlimani na kusimama mahali tambarare. Idadi kubwa ya wanafunzi wake walikuwa huko, pamoja na idadi kubwa ya watu kutoka Uyahudi na Yerusalemu, na kutoka pwani ya Tiro na Sidoni. 18Walikuja kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao. Watu waliokuwa wakisumbuliwa na pepo wachafu waliponywa pia. 19Kila mmoja kwenye hilo kusanyiko alijaribu kumgusa kwa sababu nguvu za uponyaji zilikuwa zikitokea ndani yake, na aliwaponya wote. 20Kisha akawaangalia wanafunzi wake, na kusema, “Mmebarikiwa ninyi mlio maskini, kwa maana ufalme wa Mungu ni wenu. 21Mmebarikiwa ninyi mlio na njaa sasa, kwa maana mtashibishwa. Mmebarikiwa ninyi mliao sasa, kwa maana mtacheka. 22Mmebarikiwa ninyi ambao watu watakapowachukia na kuwatenga na kuwashutumu ninyi kwamba ni waovu, kwa ajili ya Mwana Adamu. 23Furahini katika siku hiyo na kurukaruka kwa furaha, kwa sababu hakika mtakuwa na thawabu kubwa mbinguni, kwa maana baba zao waliwatendea vivyohivyo manabii.
Waraka (Mt. Saba)
22Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, ukarimu, utu wema, imani, 23upole, na kiasi. Hakuna sheria dhidi ya mambo kama hayo. 24Wale walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili pamoja na shauku na tamaa zao mbaya. 25Kama tukiishi kwa Roho, pia tutembee kwa Roho. 26Tusiwe wa kujivuna, tusichokozane kila mmoja na mwenzake, wala tusioneane wivu. 6:1Ndugu, ikiwa mtu amekamatwa katika uovu, ninyi mlio wa kiroho, mnawiwa kumrejesha huyo ndugu katika roho ya upole. Huku mkijiangalia wenyewe ili msijaribiwe. 2Mchukuliane mizigo, na kwa hiyo mtaikamilisha sheria ya Kristo.
Injili (Mt. Saba)
27Mambo yote yamekabidhiwa kwangu kutoka kwa Baba. Na hakuna amjuaye Mwana isipokuwa Baba, na hakuna amjuaye Baba isipokuwa Mwana, na yeyote ambaye Mwana ana hamu ya kumfunulia. 28Njoni kwangu, nyinyi nyote mnaosumbuka na mnaolemewa na mzigo mzito, nami nitawapumzisha. 29Jitieni nira yangu na mjifunze kutoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mnyenyekevu na mpole wa moyo na mtapata pumziko la nafsi zenu. 30Kwa kuwa nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.
Watakatifu wa siku
- Mfiadini wa Kikasisi Eliya, padri (1932)
- Mtawa Mfiadini Genadi (1941)
- Mtakatifu Sergio Mwungamaji, padri (1950)
- Watakatifu Watawa Karioni, mtawa, na mwanawe Zakaria, Wamisri (karne ya 4)
- Askofu Mtakatifu Guri, Askofu Mkuu wa Kazan (1563)
- Mfiadini Anastasio (karne ya 3)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 5 Desemba katika kalenda ya kanisa ni 18 Desemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki