Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Desemba 2026 › 16 Desemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 3 Desemba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 16 Desemba 2026
Jumatano · Wiki ya 29 baada ya Pentekoste · Sauti ya 3
Sikukuu na watakatifu
Nabii Sefania (635-605 K.K.)
Mfungo wa Kuzaliwa kwa Bwana
Mfungo: pamoja na mafuta
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
11Tuna mengi ya kusema kuhusu Yesu, lakini ni vigumu kuwaelezea kwa kuwa ninyi ni wavivu wa kusikia. 12Ijapokuwa kwa kipindi hiki mlipaswa kuwa walimu, bado kuna umuhimu wa mtu kuwafundisha mafundisho ya awali ya kanuni za neno la Mungu. Mnahitaji maziwa na si chakula kigumu. 13Kwa kuwa yeyote anywaye maziwa tu hana uzoefu katika ujumbe wa haki, kwa kuwa bado ni mtoto. 14Kwa upande mwingine, chakula kigumu ni cha watu wazima, wale ambao kwa sababu ya uzoefu wao katika kutofautisha haki na ubaya wamefundishwa kutambua jema na ovu. 6:1Kwa hiyo, tukiacha tulichojifunza kwanza kuhusu ujumbe wa Kristo, twapaswa kuwa na juhudi kuelekea kwenye ukomavu, tusiweke tena misingi ya toba kutoka katika kazi zisizo na uhai na imani katika Mungu, 2wala misingi ya mafundisho ya ubatizo, na kuwawekea mikono, ufufuo wa wafu, na hukumu ya milele. 3Na tutafanya hivi ikiwa Mungu ataruhusu. 4Kwa kuwa haiwezekani kwa wale ambao waliipata nuru awali, ambao walionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa kuwa washirika wa Roho Mtakatifu, 5na ambao walionja uzuri wa neno la Mungu na kwa nguvu za wakati ujao, 6na kisha wakaanguka - haiwezekani kuwarejesha tena katika toba. Hii ni kwa sababu wamemsulubisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, wakimfanya kuwa chombo cha dhihaka hadharani. 7Kwa kuwa ardhi iliyopokea mvua inyeshayo mara kwa mara juu yake, na ikatoa mazao muhimu kwa hao waliofanya kazi katika ardhi, hupokea baraka kutoka kwa Mungu. 8Lakini ikiwa huzaa miiba na magugu, haina tena thamani na ipo katika hatari ya kulaaniwa. Mwisho wake ni kuteketezwa.
Injili
1Ikawa siku moja, Yesu alipokuwa akiwafundisha watu Hekaluni na kuhubiri injili, makuhani wakuu na walimu wa Sheria walimwendea pamoja na wazee. 2Walizungumza, wakimwambia, 'Tuambie ni kwa mamlaka gani unafanya mambo haya? Au ni nani huyo ambaye amekupa mamlaka haya? “ 3Naye akajibu, akawaambia, 'Nami pia nitawauliza swali. Niambieni 4ubatizo wa Yohana. Je, ulitoka mbinguni ama kwa watu? ' 5Lakini wakajadiliana wao kwa wao, wakisema, 'Tukisema, 'litoka mbinguni, atatuuliza, ' Basi, mbona hamkumwamini?' 6Na tukisema; ilitoka kwa wanadamu; watu wote hapa watatupiga mawe, maana wote wanaamini kwamba Yohana alikuwa nabii. ' 7Basi, wakamjibu ya kwamba hawakujua ilikotoka. 8Yesu akawaambia, '“Wala mimi siwaambii ninyi ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya.”
Watakatifu wa siku
- Mtakatifu Mtawa Sava wa Storozhi (wa Zvenigorod) (1406)
- Mfiadini wa Kikasisi Andrea, padri (1920)
- Mfiadini wa Kikasisi Nikolao, padri (1937)
- Mtakatifu Georgi Mwungamaji (1960)
- Mtakatifu Mtawa Theodulo wa Konstantinopoli (karibu 440)
- Mtakatifu Mtawa Yohana, mnyamavu, aliyekuwa Askofu wa Kolonia (558)
- Mfiadini wa Kikasisi Theodoro, Askofu Mkuu wa Aleksandria (606)
- Mtakatifu Mtawa Georgi wa Chernika
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 3 Desemba katika kalenda ya kanisa ni 16 Desemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki