Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Desemba 2026 › 11 Desemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 28 Novemba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 11 Desemba 2026
Ijumaa · Wiki ya 28 baada ya Pentekoste · Sauti ya 2
Sikukuu na watakatifu
Mtawa Mfiadini na Mwungamaji Stefano Mpya (767)
Mfungo wa Kuzaliwa kwa Bwana
Mfungo: chakula kilichopikwa bila mafuta
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
15Kwa wote walio safi, vitu vyote ni visafi. Lakini kwa wote walio wachafu na wasioamini, hakuna kilicho kisafi. Kwa kuwa mawazo yao na dhamira zao zimechafuliwa. 16Wanakiri kumjua Mungu, lakini kwa matendo yao wanamkana. Wao ni waovu na wasiotii. Hawakuthibitishwa kwa tendo lolote jema. 2:1Lakini wewe yaseme yale yanayoendana na maelekezo ya kuaminika. 2Wazee wawe na kiasi, heshima, busara, imani safi, katika upendo, na katika uvumilivu. 3Vilevile wanawake wazee lazima daima wajioneshe wao wenyewe kama wenye kujiheshimu, na sio wasengenyaji. Lazima wasiwe watumwa wa pombe. 4Wanapaswa kufundisha yaliyo mazuri ili kuwaandaa wasichana kwa busara kuwapenda waume zao na watoto wao. 5Wanapaswa kuwafundisha kuwa na busara, wasafi, watunzaji wazuri wa nyumba zao, na watii kwa waume zao wenyewe. Inawalazimu kufanya mambo haya ili kwamba neno la Mungu lisitukanwe. 6katika namna iyo hiyo, watieni moyo vijana wa kiume wawe na busara. 7Katika njia zote jiwekeni wenyewe kuwa mfano katika kazi nzuri; na mfundishapo, onesheni uadilifu na heshima. 8Ongeeni ujumbe wenye afya na usio na dosari, ili kwamba yeyote apingaye aaibishwe kwa sababu hana baya la kusema juu yetu. 9Watumwa na wawatii mabwana zao katika kila kitu. Wanapaswa kuwafurahisha na sio kubishana nao. 10Hawapaswi kuiba. Badala yake, wanapaswa kuonesha imani yote nzuri ili kwamba katika njia zote wayapambe mafundisho yetu kumhusu Mungu mwokozi wetu.
Injili
12Hivyo akawaambia, 'Ofisa mmoja alikwenda nchi ya mbali ili apokee ufalme na kisha aurudi. 13Aliwaita watumishi wake kumi, akawapa mafungu kumi, akawaambia, 'fanyeni biashara mpaka nitakaporudi.' 14Lakini wananchi wake walimchukia na hivyo wakatuma wajumbe waende kumfuata na kusema, 'Hatutaki mtu huyu atutawale.' 15Ikawa aliporudi nyumbani baada ya kufanywa mfalme, akaamuru wale watumishi aliokuwa amewaachia fedha waitwe kwake, apate kujua faida gani waliyoipata kwa kufanya biashara. 16Wa kwanza akaja, akasema, 'Bwana, fungu lako limefanya mafungu kumi zaidi. ' 17Huyo Ofisa akamwambia, Vema, mtumishi mwema. Kwa sababu ulikuwa mwaminifu katika jambo dogo, utakuwa na madaraka juu ya miji kumi. ' 18Wa pili akaja, akasema, 'Bwana, fungu lako limefanya mafungu matano.' 19Huyo Afisa akamwambia, 'Chukua mamlaka juu ya miji mitano.' 20Na mwingine akaja, akasema, 'Bwana hii hapa fedha yako, ambayo niliihifadhi salama katika kitambaa, 21kwa maana niliogopa kwa sababu wewe ni mtu mkali. Unaondoa kile usichokiweka na kuvuna usichopanda. ' 22Huyo Ofisa akamwambia, 'Kwa maneno yako mwenyewe, nitakuhukumu, ewe mtumishi mbaya. Ulijua kwamba mimi ni mtu mkali, nachukua nisichokiweka na kuvuna ambacho sikupanda. 23Basi, mbona hukuweka fedha yangu katika benki, ili nikirudi niichukue pamoja na faida? 24Ofisa akawaambia watu waliokuwa wamesimama hapo, 'Mnyang'anyeni hilo fungu na kumpa yule mwenye mafungu kumi.' 25Wakamwambia, 'Bwana, yeye ana mafungu kumi. ' 26'Nawaambia, kila mtu ambaye anacho atapewa zaidi, lakini ambaye hana, hata kile alicho nacho kitachukuliwa. 27Lakini hawa maadui zangu, ambao hawakutaka niwe Mfalme wao, waleteni hapa na kuwaua mbele yangu. '' 28Baada ya kusema hayo, aliendelea mbele akipanda kwenda Yerusalemu.
Watakatifu wa siku
- Mfiadini Irenarko na wanawake saba watakatifu (303)
- Mfiadini wa Kikasisi Serafim, Mitropoliti (1937)
- Wafiadini wa Kikasisi Petro, Aleksi, Aleksi, Basili, mapadri, Watawa Wafiadini Rafaeli na Vikenti na Mfiadini Anisia (1937)
- Mfiadini Paraskeva (1938)
- Mfiadini wa Kikasisi Nikolao, padri (1941)
- Wafiadini Stefano, Basili, Gregori, Gregori mwingine, Yohana na wengine wengi (karne ya 8)
- Askofu Mtakatifu Theodoro, Askofu Mkuu wa Rostov (1394)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 28 Novemba katika kalenda ya kanisa ni 11 Desemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki