Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Desemba 2026 › 7 Desemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 24 Novemba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 7 Desemba 2026
Jumatatu · Wiki ya 28 baada ya Pentekoste · Sauti ya 2
Sikukuu na watakatifu
Baada ya Sikukuu ya Kuingizwa Hekaluni kwa Mama Mtakatifu Sana wa Mungu
Mfungo wa Kuzaliwa kwa Bwana
Mfungo: chakula kilichopikwa bila mafuta
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
20Kwenye nyumba ya kitajiri, siyo kwamba vimo vyombo vya dhahabu na shaba tu. Pia kuna vyombo vya miti na udongo. Baadhi ya hivi ni kwa ajili ya matumizi ya heshima na baadhi yake ni kwa matumizi yasiyo ya heshima. 21Ikiwa mtu atajitakasa mwenyewe kutoka kwenye matumizi yasiyo ya heshima, yeye ni chombo chenye kuheshimika. Ametengwa maalumu, mwenye manufaa kwa Bwana, na ameandaliwa kwa kila kazi njema. 22Zikimbie tamaa za ujanani. Ukifuata haki, imani, upendo na amani pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi. 23Lakini ukatae upumbavu na maswali ya kipuuzi. Kwani unajua ya kuwa huzaa ugomvi. 24Mtumishi wa Bwana hapaswi kugombana, badala yake inampasa kuwa mpole kwa watu wote, awezaye kufundisha, na mvumilivu. 25Ni lazima awaelimishe kwa upole wale wampingao. Yamkini Mungu aweze kuwapatia toba kwa kuifahamu kweli. 26Waweze kupata ufahamu tena na kuepuka mtego wa Shetani, baada ya kuwa wametekwa na yeye kwa ajili ya mapenzi yake.
Injili
20Alipoulizwa na mafarisayo ufalme wa Mungu utakuja lini, Yesu akawajibu akisema, “Ufalme wa Mungu sio kitu ambacho kinaweza kuonekana. 21Wala watu hawatasema, 'Angalia hapa!' au, 'Angalia kule!' kwa maana ufalme wa Mungu umo ndani yenu.” 22Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Wakati utafika ambapo mtatamani kuiona moja ya siku ya Mwana wa Adamu, lakini hamtaiona. 23Watawaambia, 'Angalia, kule! Angalia, hapa!' Lakini msiende kuangalia, wala kuwafuafata, 24kama umeme wa radi umulikao katika anga kuanzia upande mmoja hadi mwingine. Hivyo hata Mwana wa Adamu atakuwa ivyo katika siku yake. 25Lakini kwanza itampasa kuteseka katika mambo mengi na kukataliwa na kizazi hiki.
Watakatifu wa siku
- Mfiadini Mkuu Ekaterina (305-313)
- Mfiadini Mkuu Merkurio (karne ya 3)
- Mfiadini Merkurio wa Smolensk (1238)
- Mfiadini wa Kikasisi Evgraf, padri (1919)
- Wafiadini wa Kikasisi Eugenio na Mikaeli, mapadri (1937)
- Wafiadini wa Kikasisi Aleksanda, Aleksi, Yohana, Kornelio na Mitrofani, mapadri (1937)
- Mfiadini Augusta, Wafiadini Porfirio Stratelati na askari 200 (305-313)
- Mtakatifu Mtawa Merkurio, mfungaji wa Mapango ya Kyiv (karne ya 14)
- Mtakatifu Mtawa Simoni wa Soyga (1562)
- Mtakatifu Mtawa Mastridia, bikira
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 24 Novemba katika kalenda ya kanisa ni 7 Desemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki