Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2026 › 30 Novemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 17 Novemba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 30 Novemba 2026
Jumatatu · Wiki ya 27 baada ya Pentekoste · Sauti ya 1
Sikukuu na watakatifu
Askofu Mtakatifu Gregori, mtenda miujiza, Askofu wa Neokaisaria (karibu 266-270)
Mfungo wa Kuzaliwa kwa Bwana
Mfungo: chakula kilichopikwa bila mafuta
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
1Usimkemee mwanamume mzee. Bali mtiye moyo kama baba yako. Uwatiye moyo vijana wa kiume kana kwamba ni ndugu zako. 2Uwatiye moyo wanawake wazee kama mama zako, na wanawake vijana kama dada zako kwa usafi wote. 3Waheshimu wajane, wale walio wajane kweli kweli. 4Lakini kama mjane ana watoto au wajukuu, waache kwanza wajifunze kuonesha heshima kwa watu wa nyumbani mwao wenyewe. Waache wawalipe wazazi wao mema, kwa kuwa hii inapendeza mbele za Mungu. 5Lakini mjane kweli kweli ni yule aliyeachwa peke yake. Naye huweka tegemeo lake kwa Mungu. Siku zote hudumu katika sala na maombi usiku na mchana. 6Hata hivyo, mwanamke yule aishiye kwa anasa amekufa, ingawaje yu hai. 7Na uyahubiri haya mambo ili kwamba wasiwe na lawama. 8Ila kama mtu asipowatunza ndugu zake, hususani wale walioko nyumbani mwake, ameikana imani na ni mmbaya kuliko mtu asiye amini. 9Basi mwanamke aandikishwe kwenye orodha kama mjane akiwa na umri usiopungua miaka sitini, na ni mke wa mume mmoja. 10Lazima awe amejulikana kwa matendo mema, ikiwa ni kwamba amewajali watoto, au ameshakuwa mkarimu kwa wageni, au ameosha miguu ya waaminio, au alimesaidia ambao wamekuwa wakiteswa, au alijitoa kwa kazi yeyote njema.
Waraka (Mt. Gregori Mtenda Miujiza)
7Basi kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa faida ya wote. 8Maana mtu mmoja amepewa na Roho neno la hekima, na mwingine neno la maarifa kwa Roho yule yule. 9Kwa mwingine humpa imani kwa Roho yeye yule, na kwa mwingine karama ya uponyaji kwa Roho mmoja. 10Kwa mwingine matendo ya nguvu, na mwingine unabii. Na kwa mwingine uwezo wa kupambanua roho, mwingine aina mbalimbali za lugha, na kwa mwingnine tafsiri za lugha. 11Lakini Roho ni yule yule atendaye kazi hizi zote, kumpa kila mtu karama kwa kadiri ya uchaguzi wake mwenyewe.
Injili
12Yesu pia alimwambia mtu aliyemwalika, 'Unapotoa chakula cha mchana au cha jioni, usiwaalike rafiki zako au ndugu zako au jamaa zako au majirani zako matajiri, ili kwamba wao wasije wakakualika wewe ukapata malipo. 13Badala yake, unapofanya sherehe, waalike maskini, vilema, viwete na vipofu, 14na wewe utabarikiwa, kwa sababu hawawezi kukulipa. Kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki.” 15Wakati mmoja wa wale walioketi mezani pamoja na Yesu aliposikia hayo, naye akamwambia, “Amebarikiwe yule atakayekula mkate katika Ufalme wa Mungu!”
Watakatifu wa siku
- Mtakatifu Mtawa Nikoni, abati wa Radonezh, mwanafunzi wa Mtakatifu Mtawa Sergio (1426)
- Mtakatifu Mtawa Lazaro, mchoraji wa ikoni (karibu 857)
- Mfiadini Gobroni, aliyeitwa Mikaeli katika Ubatizo mtakatifu, na pamoja naye askari 133 (914)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 17 Novemba katika kalenda ya kanisa ni 30 Novemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki