Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2026 › 31 Oktoba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 31 Oktoba 2026

Jumamosi · Juma la 30 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumamosi ya Juma la 30 la Mwaka

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani

Kumbukumbu ya Bikira Maria siku ya Jumamosi · Kumbukumbu ya hiari

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Flp 1:18–26

18Kwa hiyo? Sijali, aidha njia ikiwa ni kwa hila au kwa kweli, Kristo anatangazwa, na katika hili ninafurahia! Ndiyo, nitafurahia. 19kwa kuwa ninajua ya kuwa hili litaleta kufunguliwa kwangu. Jambo hili litatokea kwa sababu ya maombi yenu na kwa msaada wa Roho wa Yesu Kristo. 20Kulingana na matarajio yangu ya uhakika na kweli ni kwamba, sitaona aibu. Badala yake, kwa ujasiri wote, kama ambavyo siku zote na sasa, natarajia kuwa Kristo atainuliwa katika mwili wangu, ikiwa katika uzima au katika kifo. 21Kwa maana kwangu mimi, kuishi ni Kristo na kufa ni faida. 22Lakini, kama kuishi katika mwili huzaa tunda katika kazi yangu, kwa hiyo sijui ni lipi la kuchagua. 23Maana ninasukumwa sana na mawazo haya mawili. Nina hamu ya kuuacha mwili na kuwa pamoja na Kristo, kitu ambacho ni cha thamani sana sana. 24Ingawa, kubaki katika mwili huu ni jambo la muhimu sana kwa ajili yenu. 25Kwa kuwa nina uhakika juu ya hili, ninajua nitabaki na kuendelea kuwa pamoja nanyi nyote, kwa ajili ya maendeleo na furaha ya imani yenu. 26Na hii italeta furaha yenu kubwa katika Kristo Yesu, kwasababu yangu itaongezeka, kwa sababu ya uwepo wangu tena pamoja nanyi.

Wimbo wa katikati

Zab 42:1–2, 4

1Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya wana wa Korah Kama ayala ayatamanivyo maji ya mto. ndivyo hivyo ninakiu yako, Mungu. 2Ninakiu yako Mungu, Mungu uliye hai, ni lini nitaonekana mbele zako? 4Mambo haya niayakumbuka ninapoumimina roho yangu: nilipoenda na umati wa watu na kuwaongoza kwenye nyumba ya Mungu kwa sauti ya shangwe na kusifu, ni wengi tulisherekea.

Injili

Lk 14:1, 7–11

1Iltokea siku ya Sabato, alipokua akienda nyumbani kwa mmoja wa viongozi wa Mafarisayo kula mkate, nao walikuwa wakimchunguza kwa karibu. 7Wakati Yesu alipogundua jinsi wale walioalikwa kwamba wamechagua viti vya heshima, akawaambia mfano, akiwaambia, 8“Wakati mnapoalikwa na mtu harusini, usiketi katika nafasi za heshima, kwa sababu inawezekana amealikwa mtu ambaye ni wakuheshimiwa zaidi kuliko wewe. 9Wakati mtu aliyewaalika ninyi wawili akifika, atakuambia wewe, “mpishe mtu huyu nafasi yako,” na kisha kwa aibu utaanza kuchukua nafasi ya mwisho. 10Lakini wewe ukialikwa, nenda ukakae mahali pa mwisho, ili wakati yule aliyekualika akija, aweze kukuambia wewe, 'Rafiki, nenda mbele zaidi.” ndipo utakuwa umeheshimika mbele ya wote walioketi pamoja nawe mezani. 11Kwa maana kila ajikwezaye atashushwa, na yeye ajishushae atakwezwa. '

Watakatifu wa 31 Oktoba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili A, mwaka wa siku za kazi II.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki