Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2026 › 13 Oktoba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 13 Oktoba 2026

Jumanne · Juma la 28 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumanne ya Juma la 28 la Mwaka

Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: kijani

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Gal 5:1–6

1Ni kwa sababu Kristo alitupa uhuru ili tuwe huru. Hivyo, simameni imara wala msinaswe tena katika kongwa la utumwa. 2Tazama, Mimi Paulo, ninawaambia kwamba ikiwa mtatahiriwa, Kristo hatawafaidia kwa njia yoyote ile. 3Tena, namshuhudia kila mwanaume aliyetahiriwa kwamba anapaswa kuwajibika kwa sheria yote. 4Mmetengwa mbali na Kristo, wale wote “mnaohesabiwa haki” kwa sheria. Mmeanguka mbali na neema. 5Maana kwa njia ya Roho, kwa imani tunasubiri ujasiri wa haki. 6Katika Kristo Yesu kutahiriwa au kutokutahiriwa hakuna maana yoyote. Ni imani pekee inayofanya kazi kupitia upendo ndiyo humaanisha kitu.

Wimbo wa katikati

Zab 119:41, 43–45, 47–48

41Ee Yahwe, unipe upendo wako usiokwisha na wokovu wako kulingana na ahadi yako; 43Usiliondoe neno la kweli mdomoni mwangu, maana nimesubiri kwa ajili ya amri zako za haki. 44Nitazitii sheria zako siku zote, milele na milele. 45Nitaenenda salama, maana ninayatafuta maagizo yako. 47Ninafurahia katika amri zako, nizipendazo sana. 48Nitaziinulia mikono yangu amri zako, nizipendazo; nitazitafakari sheria zako.

Injili

Lk 11:37–41

37Alipomaliza kuongea, Farisayo alimwalika akale chakula nyumbani kwake, naye Yesu akaingia ndani na kuwa pamoja nao. 38Na Mafarisayo wakashangaa kwa jinsi ambavyo hakunawa kwanza kabla ya chakula cha jioni. 39Lakini Bwana akawaambia, “Ninyi Mafarisayo mnaosha nje ya vikombe na bakuli, lakini ndani yenu mmejaa tamaa na uovu. 40Ninyi watu msio na ufahamu, Je yeye aliyeumba nje hakuumba na ndani pia? 41Wapeni masikini yaliyo ndani, na mambo yote yatakuwa safi kwenu.

Watakatifu wa 13 Oktoba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili A, mwaka wa siku za kazi II.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki