Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2026 › 12 Oktoba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 29 Septemba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 12 Oktoba 2026
Jumatatu · Wiki ya 20 baada ya Pentekoste · Sauti ya 2
Sikukuu na watakatifu
Mtakatifu Mtawa Kiriako, mkaa jangwani (556)
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
12Kwa hiyo basi, wapendwa wangu kama mnavyotii siku zote, Si tu katika uwepo wangu lakini sasa ni zaidi sana hata pasipo uwepo wangu, uwajibikeni wokovu wenu wenyewe kwa hofu na kutetemeka. 13Kwa kuwa ni Mungu anayetenda kazi ndani yenu ili kuwawezesha kunia na kutenda mambo yale yampendezayo yeye. 14Fanyeni mambo yote bila malalamiko na mabishano. 15Fanyeni hivyo ili kwamba msilaumike na kuwa watoto wa Mungu waaminifu wasiyo na lawama. Fanyeni hivyo ili kwamba muwe nuru ya dunia, katika kizazi cha uasi na uovu. 16Shikani sana neno la uzima ili kwamba niwe na sababu ya kutukuza siku ya Kristo. Kisha nitafahamu kwamba sikupiga mbio bure wala sikutaabika bure.
Waraka (Mt. Kiriako Mkaapweke)
22Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, ukarimu, utu wema, imani, 23upole, na kiasi. Hakuna sheria dhidi ya mambo kama hayo. 24Wale walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili pamoja na shauku na tamaa zao mbaya. 25Kama tukiishi kwa Roho, pia tutembee kwa Roho. 26Tusiwe wa kujivuna, tusichokozane kila mmoja na mwenzake, wala tusioneane wivu. 6:1Ndugu, ikiwa mtu amekamatwa katika uovu, ninyi mlio wa kiroho, mnawiwa kumrejesha huyo ndugu katika roho ya upole. Huku mkijiangalia wenyewe ili msijaribiwe. 2Mchukuliane mizigo, na kwa hiyo mtaikamilisha sheria ya Kristo.
Injili
37Hivyo, habari juu ya Yesu zilienea kila sehemu katika maeneo yanayozunguka mkoa huo. 38Kisha Yesu aliondoka katika mji huo na akaingia katika nyumba ya Simoni. Sasa, mama mkwe wake na Simoni alikuwa anaumwa homa kali, na wakamsihi kwa niaba yake. 39Hivyo, Yesu alimsogelea, akaikemea ile homa na ikamwachia. Ghafla alisimama na akaanza kuwatumikia. 40Jua lilipokuwa likizama, watu walimletea Yesu kila mmoja aliyekuwa mgonjwa wa maradhi ya aina mbalimbali. Aliweka mikono yake juu ya kila mgonjwa na akawaponya wote. 41Mapepo pia yaliwatoka wengi wao yakilia kwa sauti na kusema, “Wewe ni mwana wa Mungu!” Yesu aliwakemea mapepo na hakuwaruhusu waongee, kwa sababu walijua kwamba yeye alikuwa ni Kristo. 42Wakati kulipopambazuka, alienda eneo lisilokuwa na watu. Makutano ya watu walikuwa wakimtafuta na wakaja katika eneo alilokuwapo. Walijaribu kumzuia asiende mbali na wao. 43Lakini akawaambia, “Lazima pia nihubiri habari njema za ufalme wa Mungu katika miji mingine mingi, kwa kuwa hii ndiyo sababu nilitumwa hapa.” 44Kisha aliendelea kuhubiri ndani ya masinagogi katika uyahudi wote.
Watakatifu wa siku
- Kupatikana kwa masalia ya Askofu Mtakatifu Yohana (Maximovich), Askofu wa Shanghai na San Francisco, mtenda miujiza (ROCOR)
- Mfiadini wa Kikasisi Yohana, Askofu Mkuu wa Riga (1934)
- Wafiadini Dada, Gabedai na Kazdoa (karne ya 4)
- Mtakatifu Mtawa Theofani Mwenye Huruma
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 29 Septemba katika kalenda ya kanisa ni 12 Oktoba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki